HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 6 October 2018

BENKI YA AZANIA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

Benki ya Azania yenye matawi yake sehemu mbali mbali nchini imeadhimisha wiki ya huduma kwa mteja, lengo kuu likiwa ni kuwashukuru wateja wake kwa kuwa nao bega kwa bega katika ukuaji wa benki hiyo.
Katika maadhimisho hayo benki ya Azania imewatembelea wateja kwenye sehemu zao za kazi lengo likiwa ni kuona namna gani wanaweza kuboresha huduma zao, mbali na hilo waliweza kutoa zawadi na vyeti kwa wateja wao lengo likiwa ni kuwashukuru kwa kuichagua benki hiyo. 
Baadhi ya wateja waliopatiwa Vyeti na Zawadi kwenye maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa mteja.

Benki ya Azania imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora kulingana na mahitaji yake.  
Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa watoa huduma.

Mbali na kutoa huduma hizo Watoa huduma kwenye matawi mbali mbali ya benki hiyo waliweza kuvaa mavazi ya kitenge kuonyesha Utanzania wao. 
Katika kuonyesha ushirikiano na wateja Watoa huduma wa benki ya Azania waliweza kulishana keki na wateja. 
Benki ya Azania inaendelea kuwahimiza wananchi wote kujiunga na benki yao ili waweze kupata huduma bora na zenye ufanisi wa hali ya Juu. 
Azania Bank bega kwa bega!

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad