HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 29, 2018

NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA

NA TIGANYA VINCENT
VITUO vya kulelea na kutunza watoto yatima na wale walioko kwenye mazingira hatarishi nchini vimetakiwa kuiga utaratibu wa Kituo cha Shirika Masista wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora wa kumwekea kila mtoto mdogo mlezi na mwangalazi wake wa karibu wakati wote ili kuwafanya wasijione wapweke.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.

Alisema utaratibu unaotumiwa na Kituo hicho wa kumwakea mtoto mlezi na mwangalizi wake wa karibu ambaye siye Sista ni njia nzuri ya kuwasaidia watoto kutojiona kama yatima kwa kuwa wapweke na kuisi yule ndiye mzazi wake.

Aidha Naibu Waziri huyo alilipongeza Shirika hilo kwa malezi na huduma nzuri wanazotoa kwa watoto hao na wazee wasijiweza jambo ambalo limefanya waishi kwa furaha na ushirikiano miongoni mwao.

Alisema kazi inayofanywa na Shirika hilo ni nzuri na kubwa ambayo kimsingi ilikuwa ifanywe na Serikali lakini wao wameamua kwa upendo wao kuwalea na kuwatunza watoto ambao wamepoteza wazazi wao na wazee wasijiweza ambao wametelekezwa na ndugu zao.

Dkt. Ndumbalo aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikano kwa kadiri itakavyowezekana kwa Shirika hilo na mengine ambayo yanatunza watoto walioko katika mazingira hatarishi na wazee wasiojiweza ili nao wajione kuwa ni Watanzania sawa na wengine.

Aidha alitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kushirikiana na Serikali kuotoa misaada na kulea wazee waliotelekezwa na watoto ambao ni yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi ili nao waweze kufurahia maisha yao hapa nchini.

Alisema baadhi ya watoto hao wana vipaji mbalimbali kama watalelewa katika mazingira sawa na watoto wengine watakuwa msaada mkubwa katika nchi ambapo baadhi yao watakuwa wataalamu katika sekta mbalimbali na wengine kuwa wasanii watakaosaidia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda hapa nchini.

Naye Kaimu Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Wamisionari wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Sisita Emmanuella MC alisema kituo hicho hivi sasa kinalea wazee wasijiweza 45 na watoto 17 ambao baadhi yao ni yatima hawana mzazi hata mmoja, wengine ni wale waliokotwa baada ya kutupwa na mama zao.

Alisema baadhi ya wazee katika Kituo hicho wamekuwa wakiwa hawa sehemu ya kulala na wengine wakiwa wametelekezwa na ndugu zao bila hata msaada wa chakula.

Aidha alisema ili kuwalea vizuri watoto hao kila mmoja wao amekuwa na mlezi ambaye siye Sista kwa ajili ya kuijengea jamii uwezo wa kuwahuduma watoto wa aina hiyo katika jamii zao.

Kwa upande wa Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Tabora Baraka Makona alisema kuwa Mkoa huo umeshabaini wazee 70,020 na watoto walioko katika mazingira hatarishi 50,000.

Alisema kimsingi wamekuwa wakijitahidi kuzijengea uwezo familia za watoto walioko katika mazingira hatarishi ili waendelee kuishi zaidi katika maeneo yao zaidia kuliko kuwaweka katika vituo ili kuepuka kuwa na vituo vingi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akisalimia wazee  leomara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake. 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akimsalimia Mzee Lucas Simon(kushoto)  leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
 Kaimu Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Wamisionari wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Sisita Emmanuella MC (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(katikati) leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akikabidhi maziwa na sukari kwa Masisita mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza  kwa ajili ya kuwapa  sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad