HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 15, 2018

NAIBU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATAK WANAOPINGA MUUNGANO WASHTAKIWE KAMA WAHAINI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed ametaka kutungwa kwa sharia Maalum kwa watu watakaobeza Muungano kutajwa kuwa ni wahaini.

Ahmed Amesema hay oleo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akichangia Mada katika kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililobebwa na Mada ya ‘Falsafa ya Mwalimu Nyerere juu ya Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda Tanzania’.

“mimi ninachoomba tuvutane tu ila tuwandalie mstakabali mzuri hao wanakuja nyuma yetu na tuwajenge hawa kwa mazuri nimeguswa kidogo na katibu wa baba wa Taifa pale alipouliza nyie vipi huko katika vyama vya siasa nimekuwa nashangaa sana wanasiasa awajui kupambanua kipi cha kubeza na kipi sio cha kubeza”

Ahmed amesema kuwa kuna tatizo la kisheria katika mfumo wa kuongoza hivi vyama kwani wanasiasa ndio wamekuwa kipaumbele kuhoji muungano jambo ambalo linafanywa kwa utashi wa kulenga kupata kura tu.

Amesema ifike wakati wakusema kuwa mtu akigusa Muungano ni uhaini sio kwa kumgusa Rais Peke yake kwani wanfanya hivi kwa kutaka kupata umaharufu wa kisiasa.

Amesema ifike mahali ni sharia kufata fikra za Mwalimu kwani anayekiuka hizo atakuwa ametenda kosa kubwa la jinai kwani tukiacha uhuru tutaendelea kudanganyana siku hadi siku.
Alimaliza kwa kusema kuwa leo amekuja Rais Dk John Magufuli anasimamia haya lakini ipo siku atakuja kiongozi atayaaopuuza haya anayofanya kisha taifa hili litapromoka kwa kiwango cha ajabu nakupoteza nguvu yote hii.
 Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa mada ya Umuhimu wa Taifa huru na uhuru wa Wananchi katika kukuza uchumi wa Viwanda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigambboni Sarah Msafiri akizungumza kuhitimishaKongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere
 CAG Mstaafu, Ludovick Utouh akichangia mada katika Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Watoa mada na Wajumbe wa Meza kuu wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Viongozi wastaafu na wadau mbalimbali wakifatilia kwa karibu Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Baadhi ya Washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
Picha ya Washiriki wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad