HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 15, 2018

MSIMU MPYA WA VICHEKESHO VYA MWANTUMU KUANZA KESHO

Msimu mpya wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo huonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo unaanza rasmi Jumanne Oktoba 16, huku vikiwa vimeongezewa manjonjo ili kuwahakikishia watazamaji na mashabiki wake burudani isiyo na upinzani.

Vichekesho hivyo vinavyoongozwa na mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile maarufu kwa jina la kisanii JOTI ambaye kwenye vichekesho hiviamevaa uhusika wa watu watatu tofauti ; Mzee Mrisho, Kaboba na Mwantumu Sahare, vimekuwa ni moja wa vipindi vinavyotazamwa sana nakupendwa na maelfu ya watu hapa nchini ambapo huonyeshwa kupitia chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Majina maarufu pia katikatasnia ya uigizaji na uchekeshaji yatakuwepo msimu huu akiwemo Mzee Fungafunga (Mzee Mwalubadu), Mama Abduli (Mwantumu Mcharuko), AlexWasponga(Kayombo) na wengineo wengi

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa vichekesho hivyo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwatangu kuanza kwa msimu wa kwanza wa vichekesho vya Mwantumu mnamo Oktoba 2017, vichekesho hivyo vimekuwa na msisimko wa aina yake navimepokelewa vizuri sana na watazamaji na hivyo kuvifanya kuwa na mashabiki wengi sana.

Amesema msimu huu wa pili watazamaji wa Maisha magic Bongo na mashabiki wa Mwantumu watashuhudia mikasa ya aina yake ambapo baada ya Bahati kupata ujauzito, baba yake mzee Mwalubadu anaamua kumpeleka Kaboba katika vyombo vya sheria kwa kosa la kumpa Bahati ujauzito. Hatahivyo suala hilo linafika kwa Babu yake Kaboba mzee Mrisho, ambaye wakati huohuo hataki Kaboba apate matatizo yoyote. Kinachotokea hapo nidrama ya aina yake itakayowaacha watanzamaji wakivunjika mbavu kwa kucheka!

“DStv kupitia Chaneli yake pendwa ya Maisha Magic Bongo, siku zote imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunatoa msisitizo kwenye maudhui yandani na vichekesho hivi ya Mwantumu ni mfano halisi. Hii ni yetu, imetengenezwa hapa tanzania na wazalishaji, waandaaji na waigizaji wote wa hapahapa nchini” alisema Alpha.


Vichekesho vya Mwantumu vilianza msimu wa kwanza mnamo Oktoba 2017 Na kuendelea kwa muda wa mwaka mmoja ambapo vilikuwavikionyeshwa mara moja kwa wiki. Katika msimu huu mpya vichekesho hivyo vitaonekana mara mbili kwa wiki siku ya Jumanne na Jumatano saa mojana nusu usiku. Hii itawapa fursa mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi kwani kumekuwa na maombi mengi yakuongeza vipindi hivyo kutokana na umaarufu wake.

Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo vitakuwa vinaonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo.
Mzalishaji wa vipindi Rakim Mohamed akizungumza jinsi walivyoweza kuzalisha vipindi hivyo vya kuchekesha vya Mwantumu wakati wa uzinduzi mpya wa Vichekesho hivyo.
Mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile "JOTI" akizungumza wakati wa uzinduzi wa vichekesho vyao vya Mwantumu ambavyo vitakuwa vinaonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad