HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 4, 2018

MWENYEKITI WA BODI DAWASA AKAGUA MRADI WA MAJI CHALINZE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mwenyekiti wa Bodi ya ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA)  Mkuu wa Majeshi mstaafu  Jenerali Davis Mwamunyange  amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa mtambo na mfumo wa CHALIWASA awamu ya tatu ambao chanzo chake ni mto Wami. 

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi anatarajiwa kutembelea kazi mbalimbali za mradi ikiwemo shughuli za upanuzi wa chanzo, ujenzi wa matenki na kazi za ulazaji mabomba. 

Mradi huu unaojengwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji  kupitia na DAWASA unahusisha ujenzi wa Matenki 19, ulazaji wa mabomba ya ukubwa mbalimbali kwa kilometa 1, 203, ujenzi wa vizimba vya kuchota maji pamoja na upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji wa CHALINZE. Lengo ni kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo 900 kwa siku kutoka mita za ujazo 500.

Kazi hii itakapokamilika, wakazi waliopo maeneo ya Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga, mji na vitongoji  vya Wilaya ya Chalinze na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha katika mkoa wa Pwani watafaidika.

 Mradi pia utanufaisha baadhi ya maeneo ha Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na  maeneo ya Kizuka A na B, Ngerengere, Kinoko A and B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A na B,

Hadi utakapokamilika, mradi utagharimu dola za Marakani 41,362,023.43 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya EXIM ya India.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na MajiTaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza na wanahabari baada ya kutembelea mradi wa Chalinze ulio chini ya kampuni ya Jain Irrigation System akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo Chalinze Ridhiwani Kikwete.

Meneja Mradi kutoka kampuni ya Jain Irrigation System inayojenga mradi wa Chalinze  P. G. Rajan Wapcos akimuelezea Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange mradi mzima pamoja na matenki 19 ya kuhifadhia maji




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad