HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 16 October 2018

MIAKA 19 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA, WASOMI WATOA NENO

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

KATIKA kuadhimisha   miaka 19 tangu baba wa taifa afariki tarehe  14, Oktoba mwaka 1999 viongozi na wananchi kupitia majukwaa wamemuenzi kwa kuweka mijadala mbalimbali iliyolenga kujikumbusha yale tuliyohusiwa na baba wa taifa.

Akizungumza na Blogu ya jamii msomi na mwanahistoria Francis Daudi ameielezea sikuuu hii ya kumbikizi ya Mwalimu Nyerere hasa katika uongozi wake na uwezo wa kuunganisha makabila 120, bila vita.

 "Nafikiri kila mtanzania anaweza ongea kitu juu ya Baba wa Taifa letu, swali kama Taifa ‘tumemis’  nini toka kwa Mwalimu,
jibu linaweza lisiwe sahihi kwani Mwalimu hayupo; Na kusema angelikuwepo angelifanya hivi au vile sio sawa. Lakini ilipaswa lijibiwe tu" ameeleza.

Akieleza kuhusu mambo ambayo taifa linatamani kutoka kwa Mwalimu ni pamoja na Mwalimu kuwa  mwandishi mzuri sana wa vitabu ambapo aliandika vitabu vingi na pia alitafsiri vitabu vingine.

" Nafikiri Taifa hasa hiki kizazi chetu cha Vijana ‘ tumemis’ vitabu vipya vilivyoandikwa na Mwalimu Mwenyewe" amesema

Aidha amesema kuwa;  "Taifa limemis ile Sauti ya Ukali ya Baba wa Taifa, Ikionya na kukemea mambo yasipokwenda vizuri. Leo sauti ile tunaisikia ikikemea kupitia vyombo vya habari lakini hatunaye na
 baadhi ya mambo alionya siku nyingi yamebaki kuwa na uhalisia hadi leo. Maneno ya Mwalimu yamebaki na ‘Ukali’ wake ule ule bila kusukumwa kando na nguvu ya historia" ameeleza

Pia amesema kuwa taifa limekumbuka uadilifu wa mwalimu, kwani angekemea vikali viongozi ambao wanajisahau kuwa cheo ni dhamana. Wasiojua kuwa Uongozi ni huduma. Wasiosimamia haki na kupinga rushwa na ubadhirifu
sauti nzito ya Kibaba ingekemea vikali uvaaji mbovu wa vijana, Ungekemea mno vijana wasiopenda kufanya kazi na wanaouza mali za nyumbani ili ‘kubeti’. Nafikiri angekemea miziki isiyo na adabu!" Amefafanua zaidi.

Pia amesema kuwa Mwalimu angekemea matumizi mabovu ya Kiswahili pamoja na mazongezonge yote ya uchafuzi wa lugha.

Amesema kuwa Mwalimu atakumbukwa kwa kuwa mwana wa Afrika, Mtatuzi wa migogoro na mpenda Amani kindakindaki. Bila shaka Umoja wa Afrika na Mashirika makubwa yangemtumia zaidi katika kutatua migogoro mingi ndani ya Afrika.

Kiufupi Mwalimu angeweza kututangaza na kuitetea vizuri ile heshima nje ya mipaka ya Taifa letu.

Na ameeleza kuwa Mwalimu alipendwa na watu wa dini zote, kabila zote na rika zote. Alikuwa sio mtu wa kusita. akifanya maamuzi, Anasonga mbele na kuacha historia ihukumu. Pale alipogundua amekosea alikiri hadharani na kusema wazi ilikuwa ni KOSA.

Kuhusiana na  Misimamo na Matendo yake Mwanahistoria huyo amesema kuwa, ingekuwa ni kielelezo tosha kwa viongozi vijana ambao hatujui moja kwa moja alivyokuwa nje ya hotuba na maandishi tunayosoma
wakati Fulani, Mwaka 1994 aliombwa kuwa mgeni rasmi kwenye Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi kitaifa. Mwalimu alikataa mwaliko huo, aliwaeleza wazi kuwa hayo majukumu ya kitaifa ni ya Rais aliye madarakani, hivyo aliyestahili heshima hiyo si yeye bali ni Rais Ali Hassan Mwinyi.

 Amesema kuwa; "Nafikiri angekuwepo angeonesha kwa vitendo kiongozi jinsi kiongozi anapaswa kuenenda na ni aibu kubwa kujiita Mwanafunzi au Muumini wa Mwalimu kama matendo yako hayaakisi Fikra zake" ameeleza Francis.

Na ameshauri kuhusu kujitafakari, na kuenenda vizuri katika njia nzuri ambazo Mwalimu, Mjezi makini wa Taifa alipenda tupite kwa ustawi wetu tukikengeuka, Historia itatung’ong’a na kutuhukumu daima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad