HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 16 October 2018

Aliyekuwa Miss Ubungo asherekea siku ya kunawa mikono na wanafunzi wa shule ya msingi Umoja

Aliyekuwa Miss Ubungo 2014-2016 Diana Kato amesherehekea siku ya Kunawa mikono duniani na wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja.

Siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka

Mlimbwende huyo amekuwa anajihushisha na shughuli za kijamii katika swala zima la Upatikanaji wa Maji Safi na Salama na katika shule za Msingi amesherekea siku hii ya Kunawa mikono kwa kuwafundisha watoto Jinsi ya kunawa mikono na faida za kunawa mikono.

Pia Miss Diana Kato amekutana na changamoto mbalimbali katika shule ya Msingi Umoja iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam zikiwemo ubovu wa vyoo vya Wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja pia na kutokuwa na Maji  Salama kwa kunywa shuleni hapo.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa wamedhika mabango yanayohamasisha usafi wa mazingira katika eneo la shule wakati wa siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja wakinawa mikono ili kujilinda ma magonjwa mbalimbali wa wakati wa siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka.
Aliyekuwa Miss Ubungo 2014-2016 Diana Kato akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Umojaalipowatembelea  ili kahamasisha usafi hasa kunawa mikono kwa kutumia maji safi wakati wa siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad