Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb), (aliyesimama katikakati) na ujumbe wake ambao ni Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuia ya Madola Kanda ya Afrika (CPA - Afrika) wametembelea soko la watumwa lijulikanalo kama Stone Town Mjini Unguja.
Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA - Afrika) ikiongozwa na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai wakisikiliza maelezo kuhusiana na biashara ya utumwa katika madhabahu ya kanisa la Angalikana liliojegwa mahsusi kwa ajili ya kukomesha bishara ya utumwa wakati wa ukoloni katika eneo la Mkunazini Mjini Unguja.
Spika wa Bunge la Sierra leone Dkt Abbas Bundu( wapili kutoka kushoto) akiuliza swali wakati Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuia ya Madola Kanda ya Afrika (CPA - Afrika) inayoongozwa na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai walipotembelea katika Soko la Watumwa lijulikanalo kama Stone Town Mjini Unguja.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wapili kutoka kulia) akiwa na ujumbe wake wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuia ya Madola Kanda ya Afrika (CPA - Afrika) wakisikiliza maelezo kuhusiana na biashara ya utumwa katika eneo la Mkunazini (Stone Town) Mjini Unguja.
PICHA NA BUNGE
No comments:
Post a Comment