HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 16, 2018

CWT Kilolo chawazawadia bati walimu wastaafu

CHAMA  cha  walimu   Tanzania (CWT)  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa  kimetoa  bati   500  zenye  thamani  ya  zaidi ya  shilingi milioni 8.5 kwa   mwalimu  mstaafu  25  kama  sehemu ya  kuwaaga na  kuwapongeza kwa  utumishi  bora katika  kazi  hiyo ya  ualimu .

Akikabidhi   bati  hizo jana  wakati wa  hafla  fupi ya  kuwaaga  walimu  hao  mgeni  rasmi katika  hafla  hiyo afisa   utumishi  wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo   Josephat  Kayombo   pamoja na  kupongeza   CWT wilaya ya   Kilolo  kwa  kutambua  mchango  wa   walimu   wenzao  ambao  wamestaafu  bado  alitoa  wito  kwa  walimu   waliopo kazini  kuendelea kujituma  kufanya kazi hiyo na  kujiepusha  na  utovu  wa  nidhamu .

Kayombo  alisema   serikali  imeendelea  kuwajali  watumishi  wote  wa umma  wakiwemo  walimu na kuendelea  kulipa  stahiki  zao ambazo  wamekuwa  wakizidai hivyo  ni lazima  kwa  watumishi hao kutimiza  majukumu yao  kwa  ufanisi na  kuepuka   kuonyesha  utovu wa  nidhamu  na  jeuri  pale  mwajili  ambapo amua  kumpangia kituo kipya  cha kazi .

"  Walimu  ni  kielelezo  tosha  kwa  jamii na hakuna yeyote  anayeweza  kujisifu  kwa  mafanikio yake  bila  kutambua  mchango wa  mwalimu   hivyo ni vema  walimu  kwa  umuhumu  wenu  huo kuendelea   kulenda   heshima  yenu kwa   kuonyesha  nidhamu na  kuzingatia  kanuni  na  taratibu za  kazi  na  kujiepusha  kuwa  na  nidhamu  mbovu "  alisema  Kayombo 

 Pia  alisema    kwa  kuwa  serikali  imeendelea  kuwalipa  mafao  yao   wastaafu    ni  vema  walimu    wastaafu  kuwa makini na  wimbi la  matapeli  ambao  wamekuwa  wakizunguka katika vijiji mbali mbali  vya  wilaya ya  Kilolo  na  kuorodhesha majina ya  walimu  wastaafu  kwa  lengo la  kuwatapeli   mafao  yao  ya  ustaafu .

Alisema  kuwa  kiasi cha  fedha  ambacho  wanakipata  baada ya  kustaafu  kinaweza  kuja  kuwa msaada  mkubwa  kwao mbele ya  safari    hivyo  umakini unahitajika  kwa  kuwaepuka  matapeli  hao .

Aidha  Kayombo  aliwapongeza  walimu  wastaafu  wa  wilaya ya  Kilolo kwa  kustaafu kwa  heshima na  kuwa katika  zoezi la kuhakiki watumishi   wenye vyeti  feki  walimu hao walihakikiwa  na hadi  wanastaafu   hakukuwa na mwalimu hata  mmoja  aliyekutwa na  cheti  feki .

Kuhusu  uhamisho  wa  walimu uliofanyika  alisema  kuwa anasikitishwa na  baadhi ya  walimu  kuonyesha  kugoma  kuripoti katika  kituo  alichopangiwa  na  hadi  sasa  baadhi yao  hawajaripoti  popote  jambo ambalo  wameanza  kuwafuatilia  walimu hao .

"  Kulikuwa  na uhamisho wa aina  mbili  walimu   kutoka  sekondari  kwenda  shule za msingi  na  walimu wa  shule za  msingi   na yalitolewa  maelezo  kuwa  walimu  wa  shule za msingi  wamepungua na  sekondari  kuna  walimu wa masomo ya sanaa  ambao  walikuwa  wamezidi  na hawakuwa na kazi yoyote    ndipo  ilitolewa amri  kuwatoa  huko na  kwenda  kufundisha  shule za  msingi hapo  ndipo  ilipoleta  shida  na  kuwa  walimu  wote wamelipwa  kila  mmoja zaidi ya  shilingi 500,000 kwa  walimu  wote zaidi ya 90 "  alisema  Kayombo 

Kuwa  ila  bado  watu  wanakataa  kwenda  kuripoti kituoni  hivyo  aliwataka  walimu hao  kwenda kazini  huku  malipo  mengine   wakiendelea  kulipwa  kwa  awamu na  Halmashauri ya  Kilolo  imeendelea  kuwalipa  walimu hao .

Katibu  wa  CWT  wilaya ya  Kilolo  Antony Mang'waru   alisema  kuwa   utaratibu  huo  kutoa  mkono wa  kwaheri kwa  walimu  wastaafu  ulianza julai  mwaka 2006   na  hadi sasa  ni walimu zaidi 100 wamenufaika na  zawadi  hiyo ya  bati  kutoa  CWT na  wataendelea  kufanya  hivyo .

Kwa  upande  wake  mwenyekiti  wa CWT  wilaya ya  Kilolo  Meshacky Mpenda   alisema  wao kama  viongozi  wa walimu  wilaya    hiyo  wanapongeza  jitihada mbali mbali  zinazofanywa na  serikali iliyopo madarakani dhidi ya  walimu  na  kuwa  chama kazi yake  ni  kuendelea  kuwahimiza  walimu  kufanya kazi kwa  juhudi  zaidi .

Mpenda  alisema  pamoja na  mafanikio makubwa  katika  idara ya  walimu  wilaya ya  Kilolo na  nchini kwa  ujumla  ila  bado kumekuwepo na changamoto kubwa ya  kuporomoka kwa maadili  kwa baadhi ya  walimu  kuendekeza  ulevi  wakati wa kazi ama  kuamka  akiwa amelewa  pamoja na  baadhi yao  kuwa  watoro kazini .

Hivyo  alisema  wao kama  CWT  wataendelea  kutoa  elimu  kwa  walimu watoro na  walevi ili  kujiepusha na utovu wa maadili kwani   kanuni  za utumishi  zipo  wazi na  mwalimu anaweza  poteza kazi kwa  kutofika kazini  siku  tatu .

Akielezea  changamoto  nyingine  alisema ni  ya baadhi ya  walimu  kujihusisha  kimapenzi  na  wanafunzi kuwa  suala  hilo  limeendelea  kuota  mizizi na  kuwataka  walimu   kujiepusha na tabia   hiyo  mbaya .
Afisa utumishi  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa Joseptah kayombo (kulia)  akiwa na  viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT)  wilaya ya  Kilolo wakiwakabidhi bati  walimu  wastaafu 25  kila  mmoja bati 20.
 Viongozi wa CWT  Kilolo (kulia)  wakiwakabidhi walimu wastaafu 25 zawadi ya bati 20 kila  mmoja .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad