HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 4 September 2018

YANGA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA AFRICAN LYON JUMAPILI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaaya amesema kuwa kwa sasa timu inaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi kuu Tanzania bara kulingana na proramu za mwalimu na huu ni mwendelezo wa ushindi baada ya kuanza kwa Mtibwa.

Kaaya amesema timu imemaliza mechi za kimataifa na wachezaji wakapewa mapumziko tayari wameshaanza mazoezi ikiwa  chini ya Kocha Noel Mwandila kuangalia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zilizopita ikiwemo kucheza mchezo mwinG\gine wa kirafiki hapa Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa  baada ya kushindwa kwenda kucheza mchezo wao kirafiki dhidi ya Singida United uliotakiwa kufanyika Mkoani Kigoma hiyo inatokana na ratiba ya ligi kubadilika na awali walitakiwa wacheze na Mwadui Mkoani Shinyanga.

Amesema kuwa, kwa sasa watacheza mechi ya kirafiki siku ya Jumapili dhidi ya African Lyon ili kuiangalia timu kabla ya kuendelea na ligi kwenye mchezo wao ujao watakaocheza na Stand United katika Uwanja wa Taifa.

Kaaya amewaomba mashabiki wa kanda ya Ziwa kuwa na subira na timu yao kutokana na kushindwa kwenda kucheza ila watakapopata muda wakati nwingine.

Kwa upande wa Meneja wa timu ya Yanga Nadir Haroub ' Canavaro' amesema kuwa kwa sasa hali ya wachezaji ni nzuri wanaendelea na mazoezi kwa wale ambao hawakuitwa katika timu ya taifa wakiwa wanania ya kuuchukua ubingwa wa mwaka huu baada ya kuupoteza msimu uliopita.

Canavaro amesema amekuwa anakaa na wachezaji wake akiwa anawamasihsha kujena umoja ndani ya timu kwa ajili ya kuuchukua ubingwa wa mwaka huu pamoja na hamasa ingawa kumekuwa na changamoto mbalimbali ndani ya timu.

" wachezaji wamekuwa na umoja na wakicheza kwa kujituma, wameweka matatizo ya klabu pembeni kwani hizo ni changamoto ila watahakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu inayofuata,'amesema Canavaro.

Kwa sasa Yanga wanajiandaa mchezo wao ujao dhidi ya Stand United ambapo kwa sasa Yana wamecheza mchezo mmoja na Mtibwa kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad