HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 21, 2018

ULEGA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
NAIBU Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi mafunzo ya ufugaji wa kuku kibiashara katika jiji la Dar es salaam na kueleza mikakati ya Wizara inayolenga kuongeza uzalishaji wa sekta ya mifugo na uvuvi hasa katika kuangalia suala la chakula na lishe kwa mifugo ili kuweza kuinua kipato kwa wananchi.

Akizungumza katika ufunguzi huo Ulega ameeleza Ä·uwa sekta ya ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli muhimu za kiuchumi zinazogusa wananchi wa mjini na vijijini na zaidi ya asilimia 72 ya kaya zote nchini hufuga kuku kwa malengo ya kuboresha lishe na kipato.

Na amewataka wanawake na vijana kujikita katika ufugaji wa kuku kwani huhitaji mtaji mdogo na sekta hiyo huchangia asilimia 53 ya kipato cha kaya za wafugaji wa kuku ukilinganisha na vyanzo vingine vya mapato.

Aidha kuhusiana na mada zitakazojadiliwa katika mafunzo hayo Ulega amesema yatakayojadiliwa ni pamoja na utengenezaji na matumizi ya vyakula vya kuku, uzalishaji na upatikanaji wa vifaranga bora, uthibiti wa magonjwa na matumizi ya dawa za kuku, ujasiriamali na masoko ya kuku na mazao yake.

Sambamba na hayo kutakuwa na fursa ya uanzishwaji vyama vya ushirika, majukwaa na mitandao ya wafugaji wa kuku nchini pamoja na upatikanaji wa mikopo hususani kupitia mfuko wa vijana, wanawake,wazee na wenye ulemavu katika halmashauri zote kama mpango wa serikali unavyoeleza.

Ameeleza kuwa baada ya mafunzo hayo maarifa ya wafugaji hao yataongezeka na kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji wa kuku wa mayai hivyo hali ya kipato itaongezeka zaidi.

Aidha amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020 pamoja na mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka mitano yaani 2015/206 hadi 2020/2021 na amewataka wafugaji watumie fursa ipasavyo na kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa kuku leo katika katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wafugaji hao yaliyoandaaliwa na Wizara hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa utafiti, mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Angello Mwilawa akizungumza na wafugaji wa kuku wakati ya utolewaji wa mafunzo hayo katika kuhakikisha sekta hiyo inakuwa bora zaidi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasikiliza na kujibu maswali ya wafugaji waliohudhuria mafunzo ya ufugaji wa kuku yaliyoandaliwa na Wizara hiyo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwasiliza na kuwajibu maswali wafungaji waliohudhuria mafunzo ya ufungaji wa kuku yaliyoandaliwa na Wizara hiyo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wafugaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad