HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 21, 2018

MARIAM ULEGA AWAASA WANANCHI WAFANYE MAZOEZI KWA AFYA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mariam Ulega amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo amewaomba wafanye  mazoezi mara kwa mara  ili waweze kuepukana na magonjwa.

Aliyasema hayo katika bonanza la vijana lililoandaliwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega na Diwani wa Kata ya Tengelea Shaban Manda kwenye Jimbo la Mkuranga lililohusisha timu 11 Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumza wakati wa bonanza hilo,  Mariam Ulega alisema kuwa vijana wa kata hiyo wanatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya kujiweka sawa kiafya na kupambana na magonjwa ya mara kwa mara ikiwemo magonjwa ya presha.

Amesema kuwa, michezo inaweza  kuleta ajira kwa vijana kwa kushiriki katika michezo mbalimbali na fursa hizo zinawapatia kipato na kujikimu kiuchumi, pia kushiriki kwenye michezo kuna manufaa makubwa sana.

Mbali na hilo, alisema kwua michezo pia ni furaha huweza kukutanisha watu pamoja na kuburudika, kueleimisha, kubadilishana mawazo ikiwemo kuwakutanisha watu mbalimbali ikiwemo viongozi na kuzungumzia masuala ya maendeleo.

 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga Mariam Ulega aliweza kukakabidhi jezi seti  11 kwa timu zilizoshiriki bonanza hilo, mipira minne pamoja na baiskeli mbili kwajili ya watu wenye ulemavu wa miguu.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na wananchi wa Kata ya Tengelea wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akikabidhi baiskeli kwa  watu wenye ulemavu wa miguu leo katika bonanza la vijana  lililofanyika kata ya Tengelea wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akikabidhi set za jezi na mipira timu zilizoshiriki katika bonanza la vijana lililofanyika kata ya Tengelea wilaya ya Mkuranga.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Juma Abed akizungumza na wananchi wa kata ya Tengelea kuhusu umuhimu wa kufanya mazowezi katika bonanza la vijana lililofanyika  Tengelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad