Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda ametoa mwezi mmoja sambamba na kutopewa kazi nyingine kwa Kampuni ya Nyanza hadi pale watakapomaliza miradi walioianza.
Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua miradi ya ujenzi wa barabara za halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja inatakiwa kukamilika ndani ya miezi 15 lakini hadi sasa ni miezi 11 ujenzi hauridhishi.
"Mkataba uliosainiwa ni wa miezi 15 hadi sasa ni miezi 11 mradi unasuasu na hauridhishi" amesema Makonda
"Nnaagiza kwa halmashauri zote kampuni hii ya Nyanza isipewe kazi yoyote kwenye Mkoa wangu hadi watakapokamilisha miradi mitatu waliyoianza," ameongeza.
Mkurgenzi wa manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa kusuasua hivyo wajitathimini kwa kuwa kwenye halmashauri hiyo hawatapa nafasi.
"Nilipofika Temeke niliwaambia kwenye halmashauri yangu ujanjaujanja hakuna hivyo wajitafakari kwa kina kwani nnaweza kuvunja mkataba," amesema
Amesema fedha kwaajili miradi hiyo zipo lakini cha kushangaza kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi kinyume na mkataba.
Kwa upande wa meneja mradi wa kampuni ya Nyanza Noeli Nkinga amesema changamoto wliokutana nayo ni pamoja ucheleweshwaji wa bomba lililotakiwa kuhamishwa.
"Tulitakiwa tumalize ndani ya miezi 15 lakini tumechelewa kutokana na bomba lililotakiwa kuhamishwa ambapo halikuhamishwa kwa wakati" amesema Nkinga.
Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kutoa agizo la mwezi mmoja kwa kampuni ya Ujenzi ya Nyanza kukamilisha miradi ya ujenzi barabara ya Chang`o wilayani Temeke jijini Dar es salaam(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Mkuu wakoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambata na mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Mkurugenzi wa wilaya ya Temeke,Lusubilo Mwakabibi pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji wa DAWASA, Mhadisi Aron Joseph wakikangua miradi mbalimbali inayojengwa na DMDP leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji wa Maji wa DAWASA, Mhadisi Aron Joseph akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ziara ya kukangua miradi mbalimbali inayojengwa DMDP wilaya ya Temeke.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi barabara
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi barabara
Muonekano barabara mbalimbali.
No comments:
Post a Comment