HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 18 September 2018

MWILI WA MHANDIRI WA CHUO KIKUU DKT MISANYA BINGI WAAGWA NA KUSAFIRISHWA DODOMA KWA MAZISHI

MWILI wa aliyekuwa mtangazaji mahiri nchini na Mhadhiri wa Shule ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) iliyo chini ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi (47) umeagwa leo katika Kanisa Katoliki la Makongo Juu liliopo Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Miuji jijini Dodoma kwa ajili ya mazishi siku ya kesho.

Dkt Misanya Bingi alifariki dunia siku Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wa uhai wake alifanya kazi kwenye kituo cha Radio One ambapo alitangaza vipindi mbalimbali.

Hadi umauti unamkuta alikuwa akifundisha SJMC, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. na kabla ya hapo Misanya Bingi alikuwa mtangazaji kwenye kituo cha Radio One mwaka 1996.
Misa ikiendelea

Familia ya aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi wakiaga mwili wa mpendwa wao.Ndugu, marafiki na jamaa wakitoa heshima zao za mwisho kwenye jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika kanisa Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi mara baada ya kuagwa katika kanisa Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.
Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi likiondoka kanisani mara baada ya kuagwa katika kanisa Katoliki la Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad