HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 22, 2018

Taasisi ya Marafiki Tanzania Charity yazindua siku ya Matendo mema







TAASISI ya Marafiki Tanzania Charity yazindua siku ya Matendo mema (Good Deeds Day) ambayo kidunia itafanyika Aprili 7,2019.

Siku hii ya matendo mema itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali pamoja na huduma kwa watu wenye mahitaji katika jamii yetu.

Akizungumza katika uzinduzi wa siku ya matendo mema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye pia amechaguliwa kuwa mlezi wa Marafiki Tanzania Charity amewaomba wananchi kujiunga na Marafiki Tanzania Charity ili kuweza kufanikisha kuchangia vitu mbalimbali ikiwa pamoja na huduma kwaajili ya wahitaji katika jamii yetu.

Pia Makamba amewaomba wanamarafiki Tanzania Charity kutumia Lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka kwa kila mtanzania ili kuongeza wana marafiki Tanzania kuwa wengi zaidi.

Nae  Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi-Sinza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Padre Josephat Mhozya amehamasisha kila mtu kutenda matendo mema.

 "Kutenda matendo mema ni Ibada kwahiyo watanzania tutende matendo mema kwakuwa tukitenda matendo mema tutalipwa na mwenyezi Mungu" Amesema Mhozya.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwapa wahitaji mbalimbali hapa nchini. Uzinduzi huo umefanyika na taasisi isiyo ya kiserikali (NGOs) ya Marafiki  Tanzania Charity iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Marafiki Tanzanua Charity, Emmanuel Makundi akizungumza katika uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya wahitaji pamoja na huduma ambazo zinahitaji na wahitaji mbalimbali hapa nchini.
Mratibu wa Good Deeds Day Tanzania, Doroth Namuhisa
 akizungumza katika uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwapa wahitaji mbalimbali hapa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi-Sinza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Padre Josephat Mhozya akisali kwaajili ya ufunguzi wa mkutano wa Uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day) ambayo kidunia itafanyika Aprili 7, 2019. Siku hiyo ya Matendo Mema itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwapa wahitaji mbalimbali hapa nchini.
 Mwakilishi wa Shekh Mkuu wa Dar es Salaam akiswali kwaajili ya kufungua mkutano wa uzinduzi wa siku ya Matendo mema (Good Deeds Day)ambayo itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali kwaajili ya kuwapa wahitaji mbalimbali hapa nchini.
MwanaMarafiki Tanzania charity akizungumza katika uzinduzi wa siku ya Matendo Mema Good Deeds Day uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.





 Baadhi ya washiriki waliohudhulia katika Mkutano wa uzinduzi wa siku ya Matendo Mema ambayo itafanyika Aprili 7 ,2019 siku hiyo ya Matendo mema itahusisha huduma pamoja na vitu mbalimbali kwaajili ya wahitaji katika jamii yetu hapa nchini.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akiwa kwenye picha ya pamoja na wanamarafiki Tanzania Charity mara baada ya uzinduzi wa siku ya Matendo Mema. Siku ya matendo Mema tafanyika Aprili 7, 2019 duniani kote.
  Mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akifishwa beji ya Marafiki Tanzania Charity jijini Dar es Salaam leo. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye ambaye ni Mlezi wa Marafiki Tanzania Charity akiwa katika picha ya Pamoja na wanamarafiki Tanzania Charity mara baada ya kumaliza uzinduzi wa siku ya Matendo Mema (Good Geeds Day) uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa amikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad