HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 3, 2018

GULAMALI AENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU MANONGA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Manonga Mh. Seif Khamis Gulamali ameendelea na  ziara yake jimboni humo katika kukagua na kuangalia namna miradi ya  maendeleo  inavyoendelea kutekelezwa  kunufaisha wana Manonga.

Katika ziara ziara yake Gulamali alitembelea kituo cha afya Simbo sambamba na kukagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya sekondari Mwisi ambako ameridhishwa namna miradi hiyo inavyotekelezwa na kuwataka wasimamizi kwenda na kasi na kufanya kazi zilizo bora zaidi.

Aidha Mbunge huyo alipata wasaa wa kukutana na kamati ya Zahanati ya  Nkinga, viongozi wa CCM na wadau wengine na kuona namna ukarabati wa miundombinu katika Zahanati ya Nkinga unavyoendelea. 

Gulamali  ameahidi kutoa kiasi cha shilingi 430,000 kwa ajili ya kuvuta maji ya Uhakika kwenye Zahanati ya Nkinga ili kupunguza adha kwa wananchi wa wauguzi katika mchakato mzima wa kutoa na kupokea huduma.

Pia ameahidi kuongeza vitanda viwili vya kujifungulia katika wodi ya wazazi na kueleza kuwa suala la afya hasa ya mama na mtoto lazima ipewe kipaupele.

Gulamali alihitimisha ziara yake kwa  kufanya kikao na wachezaji pamoja na viongozi wa timu  ya Manonga Queens ambayo iliibuka kidedea kwa kuichapa  Singida Worrier kwa goli mbili, na  amekabidhi mipira miwili na  kuahidi jezi na vifaa vya michezo ambavyo ameshaagiza kwa ajili ya timu hiyo itakayowakilisha mkoa mzima wa Tabora kwenye michuano ya soka daraja la kwanza Tanzania bara kwa timu za wanawake.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali (katikati) akizungumza na kamati ya Zahanati ya Nkinga mara baada ya kuwasili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad