HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 3 August 2018

Tigo Yatoa TZS 10 millioni kwa Mshindi wa Promosheni ya Tikisa Nyavu

Tigo Tanzania imemzawadia Godfrey Njau (28), mkaazi wa Dar es Salaam anayejishugulisha na biashara ya kutoa na kusafirisha bidhaa donge nono la shilingi milioni 10, baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya ujumbe mfupi ya Tikisa Nyavu.

Huku shangwe za tukio kubwa zaidi la soka duniani kwa mwaka 2018 zikiwa zimefikia kikomo, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali ya Tigo imemtangaza Godfrey kuwa mshindi wa promosheni hiyo iliyoendana na uzinduzi wa tovuti ya Tigo ya michezo www.tigosports.co.tz

‘Mbali na kitita cha TZS 10 millioni, washindi wengine walijinyakulia zawadi nne za shilingi milioni moja kila mmoja, huku wengine wanne wakijishinda luninga za kisasa na watano wakizawadiwa simu janja,’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema alipokuwa akikabidhi zawadi kwa mshindi jijini Dar es Salaam leo.

Kupitia tovuti ya michezo ya Tigo, Watanzania walipata fursa ya kufurahia uhondo wa tukio kubwa zaidi ya mpira wa miguu kwa mwaka 2018 kwa nguvu ya mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini. Wateja pia walipokea habari na dondoo muhimu kuhusu shindano hilo kubwa zaidi la mpira wa miguu kwa mwaka 2018. Kwa kujisajili kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wateja wa Tigo walipata fursa ya kushiriki katika shindano la ujumbe mfupi wa maneno ambapo mshindi wa kitita cha shilingi milioni kumi alipatikana.

‘Tigo inajivunia kuwaletea Watanzania matukio yote ya mchuano mkubwa zaidi wa mpira wa miguu kwa mwaka 2018 moja moja kwenye simu zao za mkononi, huku wakifurahia huduma bora za kidigitali kwa gharama nafuu za intaneti kwenye mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini. Hii inaendana na sifa kuu ya Tigo ya kuwaelewa wateja na kubuni bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao,’ Woinde aliongeza.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa jumla katika promosheni ya ujumbe mfupi wa maneno ya Tikisa Nyavu iliyoendana na msimu wa soka la kimataifa, Godfrey Njau wa Dar es Salaam (kulia).
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya zawadi ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa jumla katika promosheni ya ujumbe mfupi wa maneno ya Tikisa Nyavu iliyoendana na msimu wa soka la kimataifa, Godfrey Njau wa Dar es Salaam (kulia). Katikati ni Mtaalam wa Huduma za Ziada wa Tigo, Fabian Felician.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad