HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 3 August 2018

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA MAHINDI GEREZA KUU, ARUSHA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia zao la mahindi katika shamba la mradi wa Kilimo Gereza Kuu Arusha leo Agosti 3, 2018 alipotembelea gereza hilo katika ziara yake ya kikazi. Shamba hilo linaukubwa wa hekari 150 na limelimwa katika msimu wa Kilimo mwaka 2017/2018. Matarajio ya mavuno ni zaidi ya gunia 2,500 yenye ujazo wa kilo 90(kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtiaro.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa pili toka kushoto) akikagua shamba la mradi wa Kilimo Gereza Kuu Arusha leo Agosti 3, 2018 kama inavyoonekana katika picha.
Bwana Shamba wa Gereza Kuu Arusha, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Ayub Mahai(wa pili toka kulia) akitoa maelezo ya kitaalam mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini kuhusiana na uzalishaji wa zao hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiangalia zao la maharage yaliyolimwa msimu wa Kilimo mwaka 2017/2018 na kuvunwa mapema mwezi Julai mwaka huu, kwa sasa yapo katika hatua ya upepetaji na kuhifadhiwa kwa chakula cha wafungwa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akimsikiliza Mkuu wa Oparesheni Maalum katika Gereza Kuu Arusha, Mkaguzi wa Magereza, Francis Tabu alipotembelea Gereza hilo leo Agosti 3, 2018. Kamishna Jenerali Kasike amezunguza na Maafisa na askari wa Jeshi hilo ambao wanatekeleza majukumu ya Oparesheni Maalum katika magereza ya Mkoa wa Arusha.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na askari kutoka Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza leo Agosti 3, 2018 alipotembelea Gereza Kuu Arusha(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Makao Makuu ya Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad