HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 26 August 2018

TEMESA KUSIMIKA TAA ZA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kulia na kaimu Meneja wa Kikosi cha Umeme kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Pongeza Semakuwa wakitia saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio hilo lilifanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, huo ni mradi wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kulia akifurahia jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu kushoto mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, mradi huo ni wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe kushoto akijadiliana na uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja, mradi huo ni wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kikosi cha Umeme TEMESA Mhandisi Pongeza Semakuwa, Mtendaji Mkuu Dkt. Mussa Mgwatu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Shomari Shomari na mwanasheria wa TEMESA Bi. Joyce Senkondo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Mussa Mgwatu, Mhandisi Pongeza Semakuwa, Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo Ndg. Hatibu M. Hatibu na kushoto ni Mwanasheria Bi. Joyce Senkondo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Shomari Shomari.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA ZANZIBAR)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad