HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 26 August 2018

Mkurugenzi Mkuu NSSF amtaka Mkandarasi kumaliza barabara Kigamboni kwa wakati.

Mkurugenzi Mkuu wa  shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF William Erio ametembelea daraja la Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara ya lami yenye urefu wa Kilomita mbili inayo unganisha daraja la Nyerere na barabara ya Feri - Kibada iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Akikagua barabara hiyo mwishoni mwa wiki, William Erio amemtaka Mkandarasi CRJE kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa haraka  na kuhakikisha gharama ya ujenzi hazizidi kiasi cha gharama kilicho kubaliwa kwenye mkataba wa ujenzi kati ya NSSF na Mkandarasi huyo.
Kwa upande wa Mkandarasi amepokea maelezo ya Mkurugenzi Mkuu na kuahidi kutekeleza ujenzi huo. Pamoja na kuahidi utekelezaji, Mkandarasi ameomba nyongeza ya muda kutokakana na changamoto za kupatikana kwa malighafi ya udongo hasa ile ya G15.
Gharama ya mradi huu ni Tsh 21.3 billioni ambao unahusisha ujenzi wa barabara yenye njia sita, tatu kila upande zenye urefu wa kilomita mbili kutoka mwisho wa daraja hadi kwenye makutano ya barabara ya Fery - Kibada.
Pia, ujenzi unajumuisha mzunguko wenye mita za mraba 5,762, mifereji ya maji taka na yale ya mvua, kingo za katikati ya barabara "new jersey barriers", kalavati nne za umbo la boksi na moja ya ya umbo la bomba.'
 Kaimu Meneja wa Miradi NSSF Abdon Mhando (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio (wa kwanza kushoto), wengine ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF Bw. Gabriel Silayo (wa pili kulia)

Mhandisi Jamal Mruma wa nne kulia ambaye ni Meneja mradi kwa upande wa Mkandarasi M/s. CRJE Construction akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa barabara unganishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio.

 Sehemu ya kipande cha barabara unganishi kutoka mwisho wa daraja upande wa Kigamboni kuelekea barabara ya Fery – Kibada

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad