HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 2 August 2018

MAZINGAOMBWE NI SAYANSI, WANASAYANSI CHIPUKIZI WATHIBITISHA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WANAFUNZI wa shule mbalimbali za Sekondari nchini wamekutana na kuonesha mawazo yao ya kiugunduzi kupitia taasisi ya Young Scientist (YS) na kuiomba Serikali kuwasaidia ili kufanikiwa katika kutimiza ndoto zao.

Katika hali ya kushangaza na kuvutia zaidi wanafunzi wa shule ya sekondari Vingunguti jijini Dar es salaam walionesha mazingaombwe kama vile kupoteza na kuirudisha sarafu, kujitoboa sehemu za miili yao na kudhibitisha kwamba dhana ya mazingaombwe ni sayansi na si usihiri (uchawi) kama inavyofahamika na watu wengi.

Akizungumza na Michuzi blogu mmoja wa wanafunzi hao Neema Julius ameeleza kuwa jamii itambue kuwa mazingaombwe ni sayansi inayotumika kila siku katika mazingira yetu na kwa utafiti wao wamegundua hakuna dhana ya ushirikina katika hilo.

Aidha wanafunzi kutoka shule ya sekondari Same wamegundua  umeme wa utokanao na mitetemo, sauti na upepo na wameona umeme huo utafaa katika maeneo ya vijijini kwani changamoto zake ni chache ila kutokana na vifaa na uwekezaji wameiomba serikali kutoa msaada ili waweze kukamilisha ndoto zao za kuwasaidia wananchi kupata nishati ya umeme.

Pia shule ya Sekondari ya Mtakatifu  Joseph Kolping baada ya kuona ongezeko la ajali za barabari wakaona watafute mbinu ya kudhibiti na wakaja na dhana ya matumizi ya roboti kuwa mlinzi  na mwongozaji wa watumiaji wa barabara na kuripoti kila aina ya kosa linalotendeka.

Wanafunzi hao wametengeneza roboti kwa mfumo wa taa za barabarani na kumpa majukumu ya trafiki katika uongozaji wa magari na wana malengo ya kumwekea mtambo maalumu wa kupima pombe na hadi sasa wamekamilisha nusu ya mradi huo na wanahitaji kushikwa mkono zaidi ili ubunifu huo uwanufaishe wanajamii na kupunguza jamii.

Wakieleza changamoto wanazokutana nazo ni sambamba na kokosa fedha, vifaa na ushauri wa kimawazo zaidi na wameshauri serikali na taasisi binafsi kuwa mafunzo hayo yawe endelevu, serikali ishirikiane nao katika kuhakikisha mawazo yao yananufaisha jamii na wamewashauri wanafunzi kupenda masomo ya sayansi ili kuleta gunduzi nyingi nchini.

 Mwanzilishi mwenza wa YST, Dr. Gosbert Kamugisha akipata maelezo kuhusu matumizi ya umeme wa upepo, sauti, na mtetemo kutoka kwa mwanafunzi wa Same Sekondari, Samwel Osebius.
 Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya mtakatifu Joseph Kolping, Fransisco Solomon akionesha roboti waliyoitengeneza kwa ajili ya kulinda  barabarani.
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Vingunguti, Neema Julius akieleza namna mazingaombwe yana uhalisia wa sayansi tofauti na wanajamii wanavyofikiri.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad