HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 August 2018

KITUO CHA TRENI STESHENI DAR SASA KUHAMISHIWA SHAURIMOYO

 Treni ya Pugu ikipita chini katika njia ya reli ya kati ambapo juu yake itapita reli ya kisasa itakayotumia umeme.
 Mkurugenzi Mtendani wa shirika la reli Tanzania, Masanja Kadogosa akizungumza jijini Dar es Salaam leo Augusti 28,2018 wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa shirika la reli Tanzania(TRC) kufanya ziara kwenye mradi wa reli ya kisasa, (Standard Gauge Railway )ambayo imeanzia Shaurimoyo mpaka kituo cha Soga na kuendelea mpaka Kirosa mjini Morogoro.

Baadhi ya nondo zilizosukwa kwaajili ya kutengeneza nguzo  kwaajili ya kutengeneza daraja la juu ambalo reli ya kisasa itakuwa ikipita maeneo ya Shaurimoyo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya nguzo zilizowekwa tayari kwaajili ya kutengeneza reli ya kisasa itakayopita juu ili kupisha shughuli nyingine za chini kuendelea kama kawaida katika eneo la shaurimoyo jijini Dar es Salaam mradi huo wa reli ya kisasa umekaguliwa leo Augusti 28,2018 na wakurugenzi wa bodi ya shirika la reli Tanzania kwaajili ya kujua maendeleo yake.
Picha na Avila Kakingo,lobu ya Jamii.

*Ni kuanzia keshokutwa , Mkurugenzi Mtendaji TRC azungumza
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limesema kuanzisha keshokutwa treni inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Ubungo na ile ya Stesheni Gongolamboto zote zitaishia eneo la Shaurimoyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendani wa shirika la reli Tanzania, Masanja Kadogosa amesema hatua hiyo wanaendelea kuboresha eneo la Shauri Moyo na kesho wanatarajia kukamilisha mahitaji yote muhimu na baada ya hapo hapo ndipo itakuwa Shesheni ya treni hizo sambamba na ile ya mkoani.

"Hivyo wananchi wanaotumia usafiri wa treni za Dar es Salaam badala ya kuanzia Stesheni na kuelekea Ubonga au Gongolamboto sasa watakuwa wanapanda au kushuka eneo la Shauri 
moyo,"amefafanua.

Kadogosa amesema sababu za kuhamishia Stesheni hiyo Shauri moyo ni kupisha ujenzi wa Stesheni ya Reli ya Kisasa ambayo ujenzi wake unaendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo ujenzi umefikia asilimia 22 hadi sasa.

"Kesho tunakamilisha ujenzi wa eneo hili la Shauri Moyo na kesho kutwa treni zetu zitakuwa zikianzia safari zake hapa na kumalizia hapa.Tunaomba wananchi wafahamu kuwa Stesheni tunataka kuanza ujenzi wa Shesheni ya Reli ya Kisasa.

"Ujenzi huo utafanyika kati ya miezi sita hadi nane hivyo wananchi tunaomba tuwasumbue kwa kuwahamisha.Bahati nzuri ni usumbufu wenye neema kwetu sote,"amesema.

Kadogosa amewahakikishia wananchi wanaotumia usafiri huo kwamba usalama upo wa kutosha na kutakuwa na utaratibu mzuri wa kutoa maelekezo yakiwamo ya mageti ya kuingia na kotokea.

Ameongeza kwani wanatambua licha ya kuhamishia Stesheni Shaurimoyo bado kuna ujenzi wa reli ya kisasa unaendelea, hivyo wamechukua tahadhari zote.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Profesa John Kandoro baada ya kuelezwa taarifa hizo za kuhamishwa kwa Stesheni kutoka ilipo na kuhamishiwa Shaurimoyo alitaka kufahamu usalama wa abiria , ambapo amethibitishwa na Kadogosa kwamba usalama utakuwepo.

Profesa Kondoro alifika eneo la Shaurimoyo akiwa ameongozana na wajumbe mbalimbali wa bodi yake ambao walifika hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa unaondelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad