Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka Wakufunzi wa Vyuo
vya Polisi vya Dar es Salaam na Zanzibar kuhakikisha wanawafundisha
Askari Polisi Wanafunzi waliopo katika vyuo hivyo kwa kuzingatia mitaala
iliyotolewa ili wanapotoka waweze kuwatumikia Wananchi na kupunguza
uhalifu hapa nchini.
IGP
Sirro ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika
vyuo hivyo ambapo alizungumza na Wakufunzi pamoja na Askari wanafunzi
wanaosomea vyeo mbalimbali ambapo lengo la ziara hiyo ni kukagua
muenendo wa mafunzo katika vyuo vya Polisi.
Amesema
lengo la mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo yanapaswa kutolewa kwa
weledi ili kila Askari anayehitimu aweze kupata maarifa ambayo
yatawezesha kufanya kazi za Polisi vyema jambo ambalo litaendelea
kupunguza uhalifu hapa nchini.
“Kila
mkufunzi anapaswa ahakikishe lile somo analolifundisha wanafunzi wake
wanalielewa ili kusudi kama ni Ofisa, Mkaguzi na Kiongozi mdogo ndani ya
Jeshi la Polisi anafanya kazi kwa kufuata ile misingi iliyopo” Alisema
Sirro.
Kwa
Upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam Naibu
Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutta amesema lengo la mafunzo katika
Chuo hicho ni kuhakikisha kila Askari anayatambua majukumu yake ili
kupunguza uhalifu hapa nchini na watahakikisha ukakamavu na nidhamu
inazingatiwa ili kuwa na Jeshi lenye kufuata kanuni na taratibu
zilizopo.
Naye
Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Geofrey
Kamwela amesema Chuo hicho kinakabiliwa na Changamoto mbalimbali
zikiwemo za uchakavu wa miundombinu yakiwemo majengo na bwalo la Chakula
ambapo IGP Sirro aliahidi kutuma fedha za awali kwa ajili ya ujenzi wa
bwalo la kulia chakula chuoni hapo.
Kamwela
alisema hivi sasa wanaendelea kutekeleza mradi wa kuweka mfumo wa
Tehama ambao utawezesha wanafunzi kujisomea na kupata matokeo yao kwa
njia ya mtandao jambo ambalo litawafanya kwenda kisasa katika utoaji wa
elimu chuoni hapo.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini yupo katika ziara ya kukagua mafunzo
yanayoendelea katika vyuo vya Polisi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa
mafunzo yanayotolewa yanawajenga Maofisa na Askari kufikia malengo
yaliyokusudiwa ya kupunguza uhalifu hapa nchini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa wa Polisi Kamisheni ya Zanzibar wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Vyuo vya Polisi hapa nchini kwa lengo la kuboresha elimu inayotolewa na vyuo hivyo
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiimba wimbo pamoja na
Askari wakati wa kikao chake na Askari wanafunzi katika Chuo cha Polisi
Zanzibar wakati wa ziara yake. Kulia kwake ni Kamishna wa Polisi
Zanzibar Mohamed Hassan Haji na kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha
Kamisheni ya Polisi Zanzibar Faustine Shilogile.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Mafundi wa Nguo za Polisi waliopo katika Kiwanda cha Polisi cha kushona nguo Kamisheni ya Polisi Zanzibar wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Vyuo vya Polisi hapa nchini kwa lengo la kuboresha elimu inayotolewa na vyuo hivyo (Picha na Jeshi la Polisi).
No comments:
Post a Comment