HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 6 August 2018

BENKI YA CRDB YASHIRIKI KWA KISHINDO MAONYESHO YA NANE NANE-2018 KITAIFA MKOANI SIMIYU

Benki ya CRDB imeendelea kung'ara katika maonyesho ya nanenane kitaifa yanayoendelea Mkoani Simiyu kwenye viwanja Vya Nyakabindi Bariadi. Ushiriki wa Benk ya CRDB umekonga nyoyo za wananchi kwa kuwa Benki inatoa huduma zake 'live" kwa kutumia Mobile Branch pia kwa kutumia Mawakala wake 'Fahari Huduma Wakala'.
 
Wateja wanaweza kuweka pesa ama kutoa pesa zao, Pia wananchi wanapata fursa ya kupewa maelezo kwa kina kuhusu huduma zingine zitolewazo na benki ya CRDB .kama salary advance, mikopo y awafanyakazi,simbanking, SimBanking App, QR code/Mvisa, akaunti mbalimbali.

Akizungumza katika Banda la Benki ya CRDB Meneja wa Benki ya CRDB mkoani Simiyu, Ndugu Richard Karatta ametoa wito na mwaliko kwa wateja na wananchi wote wanaotembelea maonyesho hayo kuembelea Banda la Benki ya CRDB ili kufaidika na uwepo wake thabiti ambapo imedhihirisha kuwa "Ulipo Tupo".

Kauli Mbiu ya NaneNane-2018 ni WEKEZA KWENYE KILIMO,UVUVI NA MIFUGO KWA MAENDELEO YA VIWANDA BENKI YA CRDB NI MDAU MKUBWA KATIKA HIZI SEKTA AMBAZO NI WEZESHI KATIKA USTAWI WA UCHUMI WA VIWANDA.

Na udau wa Benki ya CRDB unachagizwa na mtandao mkubwa/mpana wa matawi yake zaidi ya 260 na ATMs zaidi ya 550 na Fahari Huduma wakala zaidi ya 3300 Pia wananchi wanaweza kupata huduma za Benki kupitia Simu zao za mikononi. SimBaking, SimBanking App, Internet Banking. alifafanua Ndugu, Richard Karatta.
Wateja wakiwa kwenye Banda Benki ya CRDB kupata ufafanuzi kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na na Benki ya CRDB katika kuchochea maendeleo ya viwanda kupitia Sekta za Kilimo, Uvuvi na Mifugo katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Ofisa wa Benki ya CRDB Bi. Florence Mboli (kulia), akimueleza mteja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika Uwanja wa Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoa wa Simiyu.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Florence Mboli (kushoto), akiwaeleza wateja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, mwishoni mwa wiki.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Florence Mboli (katikati), akiwaeleza wateja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, mwishoni mwa wiki.
Wateja wakipata huduma za kuweka na kutoa fedha katika tawi la benki ya CRDB katika viwanja vya Nane Nane.Wateja wakipata huduma mbalimbali katika Bande la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
Muonekano wa Banda la Benki ya CRDB.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Petronela Beda (kushoto), akiwaeleza wateja kuhusu huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB katika Maonyesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Perpetua Sarwaty, akiwaeleza wateja kuhusu huduma zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Perpetua Sarwaty, akiwaeleza wateja kuhusu huduma zinazopatikana kwenye Banda la Benki ya CRDB.
Wateja ewakiwa katika banda la Benki ya CRDB.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad