HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 17 July 2018

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO KATI YA VYAMA VYA SIASA VYA AFRIKA NA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA (CPC) JIJINI DAR ES SALAAM

*Ahimiza hivyo kujikita kujenga uchumi imara ili wananchi wapate huduma bora

Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
UKOMBOZI wa sasa kwa vyama tawala katika nchi za Afrika  ni vema wakajikita katika katika kujenga uchumi katika sekta mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.John Magufuli wakati akifungua Mkutano wa Vyama vya siasa ambavyo vilivyopigania ukombozi kwa nchi za Kusini mwa Afrika ambapo vina uhusiano na Chama cha Kikomonisti cha China (CPC) uliofanyika leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Rais Dk.John Pombe Magufuli amesema kuwa chama cha CPC kimekuwa na uhusiano ya muda mrefu na kilisaidia ukombozi katika Afrika kwa kutoa silaha lakini sasa wamekuwa na maendeleo ambapo lazima kujifunza kutoka kwao.

Amesema kuwa nchi za Afrika zitoke katika mnyororo wa unyonyaji na kuingia katika uchumi wa kujitegemea.

Amesema kuwa nchi ya China imekuwa ikitoa msaada bila masharti na kwamba kinachofanyika maelewano na msaada unatoka.

Aidha amesema kuwa Afrika inawajibu wa kushirikiana na China kutokana na mageuzi ya kiuchumi.

Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na vivutio vya kitalii huku nchi ya kwanza ikiwa ni Brazil.

Rais Magufuli amesema kuwa kufanyika mkutano huo nje ya China na kufanyika Tanzania si kwa bahati mbaya hiyo ni kutokana na vyama vya ukombozi kamati yake ilikuwa Tanzania.

Amesema kuwa CCM ni chama kikongwe katika nchi za Afrika na kuwa Kamati ya kupigania ukombozi.

Amesema kuwa China ina miradi mingi na inafanya tangu uhusiano ulipoanza hadi leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomonisti cha China, Song Tao amesema kuwa wanaendelea kujenga mifumo ya maendeleo kwa nchi za Afrika katika mazingira ya uhusiano.

Amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano na China kwa muda mrefu pamoja na chama tawala CCM.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika kabla ya kufungua mkutano kati ya viongozi wa vyama hivyo na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao akizungumza katika mkutano huo wa viongozi wa vyama vya Siasa kutoka nchi za mbalimbali za Afrika na Chama hicho cha CPC jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally akihutubia katika mkutano huo.
Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya kimataifa na  Waziri wa Mahusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Song Tao mara baada ya kufungua mkutano huo jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad