HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 18 July 2018

MABARAZA YA WATOTO YAHIMIZWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI

Na WAMJW- Mwanza
Mabaraza ya Watoto nchini yamehimizwa kutumia elimu wanayoipata kuibua vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili kuondokana na vitendo hivyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza alipowatembelea na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.

Dkt.Ndugulile amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 takribani wanawake na watoto 41,000 walifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kati yao  13,000 wakiwa ni watoto pekee.

Ameongeza kuwa vitendo vya ukatili vimeongezeka ukilinganisha na matukio ya vitendo vya ujambazi nchini ambapo suala hilo halitakiwi kufumbiwa macho na wananchi na wadau.

Aidha Dkt. Ndugulile ametoa rai kwa wananchi hasa wazazi na watoto kutomalizana nyumbani endapo vitatokea vitendo vya ukatili katika familia zao bali kuviripoti katika mamlaka husika.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Joel Festo ameishukuru Serikali na wadau kawa kuendelea kuwajali watoto kuanzia katika utoaji wa huduma za afya na kutekeleza upatikanaji wa haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa.

Dkt Ndugulile pia ametembelea na kujionea shughuli zinazotolewa na Kituo cha utoaji Huduma za pamoja kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia (One Stop Centre) hapo mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure Dkt. Bahati Peter Msaki amesema kuwa Kituo cha utoaji Huduma kwa wahanga wa ukatili (One Stop Centre) kimekuwa msaada mkubwa kwa wanajamii kwani wahanga wengi wa vitendo vya ukatili wamekuwa wakipata huduma kutoka katika kituo hicho.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akihojiwa na wanahabari watoto wa mkoa wa Mwanza wakati alipowatembelea Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo.
 Makamu Mwenyekiti Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisoma risala kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile kuelezea utekelezaji wa kazi za Baraza la Watoto kwa Mkoa wa Mwanza.
 Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Joel Festo akiishukuru Serikali na wadau kawa kuendelea kuwajali watoto kuanzia katika utoaji wa huduma za afya na kutekeleza upatikanaji wa haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushirikishwa na kutobaguliwa.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akimkabidhi Mtunza Hazina wa Baraza la watoto la Mkoa wa Mwnzxa kiasi cha Shillingi 250,000/= ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya ununuzi wa printa kwa ajili ya shughuli za ofisi za Baraza hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kitaifa wa Baraza la Watoto na Viongozi na wajumbe wa Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza, viongozi wa mkoa na wadau wa watoto mkoani humo mara baada ya kulitembelea Baraza la Watoto la Mkoa wa Mwanza na kuona shughuli wanazofanya wajumbe wa Baraza hilo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad