HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 13 July 2018

HAPA KAZI TU YAMRUDISHA LETICIA CCM

Na Khadija Seif , Globu ya jamii.

Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Leticia Ghati Mosore  pamoja na wajumbe wenzie wanne wamerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta chachu ya maendeleo.  

Leticia  amebainisha sababu mbalimbali zilizowafanya kuhama chama cha hicho na kupongeza utawala wa awamu ya tano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuona mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo na kiutendaji.

Mwenyekiti huyo amesema "utendaji wa serikali ya Sasa unatendeka Kwa uwazi, ukusanyaji wa mapato ni mzuri ,na hadi Sasa hivi imenunua ndege Kwa Kodi za watanzania na imejenga barabara za juu "fly overs" pamoja na kujenga reli ya kisasa ".  

Amefafanua zaidi na kusema serikali iliyopo madarakani imeweza kuwajali wananchi wake kwa kupeleka dawa hospitali zote nchini, imesambaza umeme vijijini kwa mradi wa umeme wa Vijijini ( REA) hayo yote yanatokana na ukusanyaji wa mapato kuwa mzuri .

Ameeleza kuwa upande wa vyama vya upinzani hawazioni juhudi hizo na zaidi wamekaa na kuponda jitihada za serikali huku wakipinga  bajeti isipitishwe huku maendeleo yakiwa yanaonekana Kwa macho.

Leticia amefafanua kuwa wameamua kuhama chama cha NCCR Mageuzi   Kwa ridhaa yao wenyewe na kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Magufuli.

Waliohama chama hicho ni pamoja na Katibu wa chama hicho Kata ya Segerea Lilian Kichunga,Katibu wa Chama cha Wanawake Mossy Kichau, Mwenyekiti wa Jimbo la Segerea Yunes Zacharia pamoja na Mjumbe Vidaline Nicholaus.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad