HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 13, 2018

DKT TIZEBA AWAPIGA MSASA WATAFITI MARUKU, BUKOBA

Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera
UONGOZI wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) umetakiwa kuongeza ufanisi katika utaalamu wao ili kuwanufaisha wakulima kote nchini kwani kwa sasa Benki ya Tafiti zilizopo hazijatumika ipasavyo.


Wataalamu wa utafiti wamepaswa kufanya vizuri pia katika eneo la kutangaza tafiti zao ikiwemo Kuongeza ujuzi katika Utafiti wa Mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na zao la kahawa ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa miche.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa taasisi hizo za utafiti sambamba na uongozi wa chuo cha mafunzo ya Kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini.

Waziri huyo wa kilimo aliwasihi watafiti hao Kuendelea kufanya juhudi kubwa kuandika miradi mbalimbali (Reseach Proposals) kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendelezaji wa utafiti kwani bajeti ya serikali pekee haiwezi kutosha kukamilisha kila changamoto zinazowakabili.

Alisema wataalamu hao wanapaswa kufanya tafiti kwa kuendana na matakwa ya sekta ya kilimo na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ili kuongeza tija katika uzalishaji wa Kahawa nchini sambamba na Mazao mengine.

Aliwasihi kuongeza ushirikiano ili kuendelea na utafiti kuhusu njia bora za uzalishaji mazao, urutubishaji udongo, mfumo wa usambazaji wa teknolojia, masoko yenye tija, tathmini ya uenezaji wa teknolojia na mchango wa matokeo ya utafiti katika kuboresha hali ya maisha ya wananchi na uchumi wa taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa kituo cha utafiti wa kilimo kinapaswa kuendelea na juhudi za uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali kama vile maharage, viazi vitamu, muhogo na mengineyo.

Kituo cha utafiti wa kilimo cha Maruku (TARI-MARUKU) ni kati ya vituo viwili vya utafiti wa kilimo katika Kanda ya ziwa ambapo makao makuu yake yapo Ukiriguru-Mwanza ambapo kinatoa mafunzo na ushauri kwa wakulima na wadau mbalimbali wa kilimo juu ya teknolojia mbalimbali za kilimo.

Katika hatua nyingine Waziri Tizeba amemuagiza Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kilimo Maruku Ndg Laurent Mathew Luhembe ndani ya mwaka mmoja kutatua changamoto ya ukosefu wa bweni la chakula.

Aliongeza kuwa chuo hicho kinapaswa kubuni mbinu mbadala za mapato ikiwa ni pamoja na kujenga kitalu nyumba (Green House) kwani itasaidia kuongeza kipato mahususi na hatimaye chuo kujiendesha badala ya kutaka changamoto zote zitatuliwe na serikali.

Aidha, Taasisi hizo za utafiti ikiwa ni pamoja na Chuo cha Maendeleo ya kilimo Maruku zimetakiwa kuhakikisha wanatunza ardhi yao ili kuondosha hofu ya uvamizi wa maeneo.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) na Uongozi wa chuo cha mafunzo ya kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018. (Picha zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba mbegu za maharege zinazofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watendaji wa Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, Taasisi ya utafiti wa kahawa (TACRI) na Uongozi wa chuo cha mafunzo ya kilimo MARUKU katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018. 
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba mbegu za maharege zinazofanyiwa utafiti na Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Maruku, wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika kijiji cha Butairuka Kata ya Maruku Wilayani Bukoba vijijini, Leo 13 Julai 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad