HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 31 July 2018

GULAMALI AHIDI KUTOA WASOMI MANONGA, ATOA FURSA KWA WANAFUNZI

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali imeendelea kutoa hamasa kwa Wanafunzi wa Sekondari kwa kuwalipia Ada Wanafunzi wanaofaulu na kuendelea na Masomo ya Kidato cha Tano na Sita.

Akizungumza na Michuzi Blogu kuhusiana na namna anavyotoa hamasa hasa katika suala la elimu Jimboni humo Gulamali ameeleza kuwa licha ya kujenga na Kuboresha Shule za Kidato cha Tano na Sita Amekuwa na Utaratibu wa kuwalipia Ada kwa Wanafunzi wanaofanya vizuri katika Mitihani yao ya Kidato cha Nne kwa kupata Daraja la Kwanza na la Pili.

Ameeleza kuwa ni Mwaka wa 3 sasa anawalipia Wanafunzi wote wanaofaulu kidato cha Nne kwenda Cha Tano na Mwaka huu zaidi ya Wanafunzi 140 wamenufaika na kusomeshwa na ofisi ya Mbunge, utaratibu huo umekuwa unatoa hamasa zaidi kwa Wanafunzi walioko Mashuleni  kwa kuweka juhudi zao katika masomo ili nao waweze kunufaika.

Akieleza malengo ya fursa hiyo Gulamali amesema kuwa suala la Elimu katika Jimbo la Manonga ni la muhimu na amedhamiria kuzalisha wasomi wengi zaidi kutoka Jimboni humo na ametoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa zinazotolewa na Serikali ili kuweza kufikia malengo.Utaratibu huu umekuwa Kivutio hamasa kwa Wanafunzi kusoma zaidi na kupata nafasi hizo za Mbunge, lakini pia umewasaidia Wazazi ambao  hushindwa kumudu Gharama za Watoto wao wanapochaguliwa  kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano hali inaowalazimu watoto hao kukatisha Masomo yao.

Miezi kadhaa iliyopita Gulamali alifungua shule ya Sekondari Ziba kwa ajili ya kidato cha Tano na Sita na bado Ujenzi wa Shule nyingine nyingi unaendelea na hii ni katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Serikali kwa kuendelea na Ujenzi wa Shule za  Sekondari kwa Kidato cha Tano na Sita kwa kila Tarafa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad