HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 18 July 2018

CHINA YAITUMIA TANZANIA KUZINDUA TEKNOLOJIA MPYA

*Ni ya mwamvuli unaotumia mionzi ya jua kutengeneza umeme, kuanza kutumika Karagwe

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
CHAMA cha Kukuza Uhusiano kati za Tanzania na China umefanikisha kupatika kwa msaada wa miavuli 100 inayotumia nguvu ya jua kuzalisha umeme ambayo imekabidhiwa kwa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.

Miavuli hiyo ambayo ni teknolojia mpya iliyozinduliwa China inakwenda kuanza kutumika wilayani humo kwenye baadhi ya shule, zahanati na kituo cha afya kwa lengo la kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana kwa ustawi wa maendeleo ya nchi yetu.

Msaada huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Taasisi ya Maendeleo ambayo ipo chini ya Chama cha Kikomunisti cha China(CPC).

Hivyo Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa CPC Song Tao ndio aliyokabidhi msaada huo ambapo amesema wanatambua urafiki , udugu na ujamaa wa nchi hizo mbili na hivyo wanatambua umuhimu wa kuendelea kuisaidia Tanzania.

Akizungumzia msaada huo Katibu Mkuu wa Chama cha Kukuza Uhusiano wa Tanzania na China Joseph Kahama amesema msaada huo umetokana na jitihadaza chama chao katika kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo mbili unaendelea.

Amefafanua kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kuzinduliwa kwa teknolojia hiyo ambayo kwa hapa nchini itakwenda kuanza kutumika wilayani Karagwe.

Amesema miavuli hiyo ya jua itasaidia kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma katika shule ambazo msaada utapelekwa na kufafanua kuwa giza litakapoingia basi wafunzi watapata mwanga kupitia msaada huo.

Pia amesema kwenye vituo vya afya na zahanati  msaada huo unakwenda kusaidia kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya na kueleza miavuli hiyo inaweza kutumika katika vifaa mbalimbali vinavyotumia umeme.

"China imeamua kuitumia Tanzania kuzindua teknolojia hiyo ambayo haiko mahali kokote duniani .Tumepewa miavuli 100 na mingine itaingia nchini Oktoba mwaka huu .

Alipoulizwa kuhusu thamani ya msaada huo amejibu kuwa hawezi kuifahamu ila anachojia teknolojia mpya nayo ina gharama zake.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Kukuza Uhusiano wa Tanzania na China Dk.Salim Ahmed Salim ameipongeza nchi ya China kwa msaada huo na ni uthibitisha unaodhihirisha urafiki wao wa muda mrefu.

Dk.Salim amesema Tanzania inatambua mchango na misaada inayotolewa na Jamhuri ya Watu wa China na kuongeza Rais Dk.John Magufuli amethibitisha kwa vitendo kuhusu kutambua na kuuenzi uhusiano wa nchi hizo mbili.

Amesema China imekuwa mstari wa mbele katika kila hatua na lengo lake ni kuona inashiriki katika jitihada za maendeleo na msaada wa leo ni uthibitisho wa uhusiano mzuri.

Kwa upande wa katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe Innocent Nsena amesema wamepokea msaada huo kwa mikono miwili n umekuja kwa wakati muafaka kwani unakwenda kuboresha mazingira ya kusomea na kufafanua wilaya ya Karagwe iko pembezoni hivyo jukumu lililopo ni kutengeneza mazingira mazuri.

Amesema kuwa msaada huo utakwenda kwenye shule zisizopungua 10 , kituo cha afya kimoja na zahanati moja.

Kuhusu changamoto ya nishati ya umeme amefafanua sio kubwa Serikali imeendelea kuhakikisha inasambaza umeme vijijini kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini(REA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad