HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 21 June 2018

Veteran wa Liverpool atua Dar kwa mwaliko wa Standard Chartered

Na Mwandishi Wetu
Sami Hyypia veteran wa timu ya Liverpool yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered.
Mchezaji huyo mwenye haiba ya aina yake aliwasili nchini Jumanne, kuhudhuria michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kuanza jumamosi wiki hii.
Akizungumza klatika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema benki yake imefurahjishwa sana na ujio wa mchezaji huyo wa zamani.
“Tumefurahi sana kuwa na Sami nchini na kumshirikisha katika michuano ya tatu ya kombe la Standard Chartered . Sami pia atatumia uwepo wake kufanya kazi na timu ya vijana chini ya miaka 17– Serengeti Boys”
Sami Hyypia ni mmoja wa viungo hatari ambao walivaa fulana nyekundu wakati wa utawala wa makocha Gerard Houllier na Rafael Benitez na kumfanya kuwa mmoja wa walinzi hodari barani Ulaya.
Mchango wa Hyypia katika soka la England kulimfanya atambuliwe kwao (Finland) kwa kupewa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka saba. (1999, 2001, 2002, 2003, 2005, 2006 na 2008).
Baada ya kusaidia timu yake dhidi ya Sheffield Wednesday  hapo Agosti 7, 1999, Hyypia akawa katika mahusiano mazuri ya kisoka na Stephane Henchoz na kuwa na viungo bora wa ulinzi 2000-01.
Aidha uchezaji wake na Jamie Carragher ulitengeneza kitu kilichokubalika kuwa ngome thabiti  baada ya Liverpool baada ya kutwaa Champions League katika viwanja vya Ataturk.
Hyypia ndiye aliyefunga goli la kukumbukwa sana wakati alipofunga goli dhidi ya Juve katika robo fainali.
Historia ya soka, alisema mtendaji huyo wa Benki, itamweka katika eneo zuri kabisa la kibiashara mchezaji huyo ambaye wapenzi walimweka katika orodha ya kuwa mtu wa 38 kati ya watu 100 waliofanya vyema katika klabu hiyo.
Akiwa nchini pamoja na kufanya kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys atakutana na vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wenye akaunti katika benki ya Standard Chartered.
Sami pia atahudhuria michuano ya Standard Chartered  inayoanza Dar es salaam Jumamosi hii.
Michuano ya soka ya Standard Chartered hufanyika kwa kila mchezo kutumia dakika 10 na mshindi atapata zawadi ya kwenda Anfield kuiona klabu ya Liverpool.
Michuano hii ya tatu nchini Tanzania toka ianzishwe mwaka 2005 itashirikisha timu 32 zinazotokana pia na wateja wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Salum Madadi, katika mkutano huo na waandishi wa habari aliishukuru benki ya Standard Chartered kwa kusaidia kukuza michezo na hasa soka.
Naye kocha wa Serengeti Boys, Bw. Oscar Mirambo aliipongeza benki hiyo kwa kumleta Sami Hyypia nchini Tanzania na kusema itakuwa ni fursa nzuri kwa timu ya Serengeti kuwa naye
Akizungumza kuhusiana na  ziara yake na uzinduzi wa michuano hiyo akishirikiana na Waziri wa Habari, Sanaa, Wasanii na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, gwiji huyo wa Liverpool, Hyypia alisema kuwa amefurahi kuhudhuria mashindano hayo na kufika kwa mara ya kwanza nchini huku akitoa wito kwa  wachezaji wenye vipaji wa Afrika pamoja na Tanzania kujitahidi ili kupata fursa ya kucheza soka la kulipwa nchini Uingereza na nchi nyingine.
Hyypia amesema kuwa kwa sasa kuna wachezaji wengi wenye vipaji ambao wanatamba Uingereza kutokana na kuongeza bidii.
Amesema kuwa tokea enzi ya Tony Yeboah ambaye alicheza naye, kwa sasa kuna wachezaji kama Sadio Mane, Mohamed Salah na wengine wengi wanaotamba katika ligi mbalimbali barani Ulaya na mabara mengine.
Amesema kuwa atafanya mazungumzo na Shirikisho la Kandanda nchini (TFF) kupitia benki ya Standard Chartered ili kuona namna ya kuwawezesha wachezaji wa Tanzania kucheza soka nchini Uiengereza na nchi nyingine kama Finland.
“Kwa sasa nipo nchini na bahati nimekutana na viongozi wa TFF hasa kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi, pia nitakutana na Waziri wa Michezo, nini kitafanyika, naomba msubiri,” alisema Hyypia.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akiwa ameongozana na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Gwiji huyo wa Liverpool nchini. Wengine katika picha nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akifurahi jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (katikati) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akipeana mkono na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia mara baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akipeana mkono na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (kulia) mara baada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad