HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 21, 2018

MKAPA AVUNJA UKIMYA WANAOSUBIRI KUMWAGIWA FEDHA KWA AJILI YA MAENDELEO

*Asema heshima ya nchi ni kujitegemea

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amesema hakuna Mtu wa kutumwagia fedha kwa ajili ya maendeleo yetu, bali yataletwa kwa watu kufanya kazi na heshima ya nchi ni kujitegemea .

Mkapa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua kitabu cha Hali ya umasikini hasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na Afrika kwa ujumla.

Kitabu hicho kimeandikwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi Martin Lumbanga. Kitabu hicho kimepewa jina la Global Poverty(The Case for Sab-Sahara Afrika)

Kabla ya kuzindua Kitabu hicho Mkapa amesema "Huu utamaduni wa kusubiri kumwambiwa fedha sijui umetoka wapi.Haipo hata katika Chama tawala ya kumwagia pesa."

Akasisistiza kwa kuhoji tena kwa Dunia hii ya Trump? "Lazima tufanye kazi kwa maendeleo yetu badala ya kusubiri fedha kutoka nje,"amefafanua Mkapa.

Mkapa anasema inashangaza unaposikia wapo wanaosubiri kumwagiwa fedha tena utasikia "Neema yaja .Haipo, heshima ya nchi ni kujitambua na kujitegemea."

Kuhusu kitabu hicho amempongeza Balozi Lumbanga kwa kuandika kitabu hicho na kumuelezea ni mtu makini na anayemfahamu vema kwani amewahi kufanya naye kazi.

"Mafanikio yangu wakati ule nikiwa madarakani yalichangiwa sana na Balozi Martin Lumbanga,"amesema.

Akizingumzia kitabu hicho Balozi Lumbanga amesema ameamua kuandika kitabu hicho kutokana na kuona hali ya umasikini iliyopo.

Hivyo kupitia kitabu hicho anaelezea umuhimu wa kwanza kukubali umasikini upo kwa nchi za Afrika na kisha kuangalia namna gani ya kuondokana nao.

"Kupitia kitabu hiki nimeelezea kwa kina kuhusu hali ya umasikini.Na ambacho nimeeleza kwanza lazima tukubali kuwa umasikini upo na hatua gani za kuchukua.

"Kwa bahati nzuri nchi nyingi za Afrika zinajitambua kuwa ni maskini na kazi inayoendelea ni kuondokana na huo umasikini na maendeleo yanaonekana,"amesema.

Amefafanua kitabu hicho alianza kukiandika wakati akiwa masomo akichukua PHD mwaka 2009 nchini Uswis na hata baada ya kurudi nchini Tanzania aliendelea kukiandika na hatimaye leo kimezinduliwa.

Kitabu hicho kina kurasa 248 na kimechapishwa na Kampuni ya Uchapishaji ya Mkuki na Nyota chini ya Mkurugenzi Mtendaji Walter Bgoya.Kampuni hiyo imekuwa ikichapisha vitabu kwa mwaka 46 sasa.
Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akizundua kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) pamoja na Mtunzi wa kitabu hicho Balozi Martine Lumbanga (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya(kulia), uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
 Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
 Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akionyesha kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) mara baada ya kukizindua kushoto ni Mtunzi wa kitabu hicho Balozi Martine Lumbanga na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya, Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akipokea zawadi ya kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) na Balozi Martine Lumbanga mara baada ya Uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
 Mtunzi wa kitabu hicho Balozi Martine Lumbanga (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya, katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
Balozi Martine Lumbanga(kulia) akisaini kitabu cha mmoja wa wageni waliofika kwenye uzinduzi huo baada ya kukinunua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad