HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 27 June 2018

UMOJA wa Mataifa (UN) umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia vizuri mipango ya Malengo ya Milenia ikiwemo ya kukuza Uchumi.

Hayo yamesemwa J na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez wakati wa mkutano wa kubadilishana mawazo juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) kati ya Serikali ya Tanzania, Zanzibara, wadau wa idara mbalimbali za Serikali, Vyuo vikuu, Taasisi za Kijamii pamoja na Shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

Akizindua rasmi mkutano huo, Alvaro Rodriguez ameweka wazi kuwa, Nchi ya Tanzania imeweza kuanza vizuri  katika malengo hayo huku ikianza kufanikiwa kiuchumi.

“Kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia,Tanzania imefanya vizuri kwenye uchumi. Kwa sasa wanatakiwa waongeze juhudi zaidi kwenye malengo mengine ambayo hawajafanikiwa ili wafanikiwe.

Mkutano huu unafungua milango kwa Tanzania ili kuweza kufikia malengo zaidi ya Milenia ” Alieleza Alvaro Rodriguez.

Alvaro ameongeza kuwa, mkutano huo umekuja muda sahihi kwao na wadau hao ambao ni Serikali kwenye malengo ya Maendeleo endelevu ya Dunia huku wakitarajia Tanzania mpaka kufikia 2030 watafanikiwa kwenye malengo yote ikiwemo Elimu, na Suala la Mabadiliko ya Tabia Nchi ambalo limekuwa kikwazo kikubwa kwa jamii ikiwemo vijana wa kike na kiume.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Faustine Kamuzola ambaye alikuwa  mmoja wa waendesha mada kwenye mkutano huo, ameeleza kuwa Tanzania imefanikiwa katika uchumi wake huku pia ikiweza kulinda masuala ya Kimazingira.

“Kwa sasa tumefanikiwa kufika uchumi unaokuwa. Kupitia Mazingira kwa sasa tunatakiwa tutumie Sayansi ya Mazingira katika kuboresha  vitu vinavyoleta athari na vibadilishwe kisayansi ili vije kutumika katika kukuza uchumi wa watu wake” Ameeleza Dk. Kamuzola.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema Tanzania ni kati ya nchi zote Duniani ambazo zimekubali kufuatilia malengo yote ya Dunia, Malengo yote 17 ambapo kila nchi imejiwekea mipango yake ya namna ya kufuatilia hivyo kwa sasa wanapitia uratibu uliopo kwa sasa ili kujipima wahakikishe wanafikia malengo.

"Ndani ya Serikali yetu tunaweka utaratibu vizuri. tunaamini baada ya mkutano wetu wa leo tutakuwa na upana zaidi wa kushughulikia malengo haya.

Kwa mpango huu wa SDGs Tanzania imeweza kuweka mikakati katika mpango wa maendeleo ya miaka mitano ya masuala ya kukuza uchumi huku kwa Zanzibar tukitumia MKUZA. Mpango huu ulianza kutumika awali na kwa sasa tunaenda nao ambapo tunaangaliai uchumi zaidi ikiwemo thamani ya bidhaa zinazodharishwa nchini, Mazingira, Usawa wa kijinsia, Kilimo na mengine mengi" alieleza Balozi Mushy.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez  akifungua mkutano wa kubadilishana mawazo juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) kati ya Serikali ya Tanzania, Zanzibar, wadau wa idara mbalimbali za Serikali, Vyuo vikuu, Taasisi za Kijamii pamoja na Shirika hilo la Umoja wa Mataifa.
 Mmoja wa washiriki kutoka mashirika binafsi akichangia nada katika mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali hapa nchini.
 Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kutoka kushoto) akiwa ameshika mpira na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy(kulia),  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda  na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Bi. Halima Maulid Salum(kushoto)  
 Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kubadilishana mawazo juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) kati ya Serikali ya Tanzania, Zanzibar, wadau wa idara mbalimbali za Serikali, Vyuo vikuu, Taasisi za Kijamii pamoja na Shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad