HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 27, 2018

WILFRIED BONY AOMBA WARUHUSIWE KUPIGA PICHA KATIKA VIVUTIO ILI KUITANGAZA TANZANIA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Swansea City ya nchinu Uingereza Wilfried Bony akamatwa na polisi baada ya kupiga picha feri.

Bony alikamatwa na polisi baada ya kupiga picha kwenye pantoni feri wakati hairuhusuwi  kupiga picha na kuachiwa baadae.

Mshambuliaji huyo alikuja nchini kwa ziara binafsi ikiwemo kufungua  kituo cha michezo , burudani pamoja na kusaidia watoto yatima hususani wanaoishu na ugonjwa wa upungufu wa damu (selimundu).

Akizungumza na Globu ya Jamii, Bony ameiomba  serikali ya Tanzania itoe fursa kwa wageni  wanapofika nchini kupiga picha ili kuweza kutangaza vivutio vya Utalii duniani.

 Bony amesema kuwa alipata msukosuko wa kushikiliwa na wanausalama akiwa katika pantoni Ferry baada ya kupiga picha ambapo kikawaida hairuhusiwi kufanya kitu hicho.

"Niliambiwa niwafuate baada ya mimi kupiga picha katika pantoni, sikuwa nafahamu kama siruhusiwi kupiga picha ila kwa upande wangu napenda kuwaomba serikali waruhusu watu hususani wageni wapige picha na kutangaza vivutio vilivyopo Tanzania,"amesema Bony.

"Nimepata changamoto nyingine nikiwa katika mbuga ya wanyama Mikumi nilikataliwa kupiga picha kabisa ila nipate fursa ya kutangaza vivutio hivyo na kama tukija watu wengi basi nchini itakuwa imetangazwa zaidi na watalii kuongezeka,"

Amesema kuwa, anatarajua kurudi tena nchini kwani ameamua kuja kuwekeza nchini kwenye michezo, burudani na kuendelea kutoa misaada kwa watoto yatima na wanaosumbuliwa na ugonjwa wa upungufu wa damu (selimundu).

Kwa upande wa mwenyeji wake Yasmine Razaq amesema kuwa anaomba serikali iweze kuondoa vikwazo mbalimbali kwa wageni ili waweze kutangaza utalii wetu duniani ikiwemo kupiga picha kwenye maeneo yanayoweza kuvutia watalii.

Mbali na hilo amepanga kuwaleta wachezaji wengine nchini kutoka Ligi Kuu ya Uingereza kwa ajili kusaidia uwekezaji wa michezo hususani watoto wadogo.

Kampuni ya Asas Diaries waliowezesha mkutano huo wa waandishi wa habari, Msimamizi wa kampuni hiyo Fahad Alli amesema wameamua kutilia mkazo kauli ya serikali ya Hapa Kazi Tu kwa kuamua kujiwekeza kwenye kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo burudani na michezo na tayari wameanza kwa Ali Kiba na Samatta.
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na timu ya Swansea City ya Uingereza Wilfried Bony akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wake uliofanyika leo akielezea madhumuni ya safari yake ya kuja Nchini Tanzania,kulia ni mwenyejiw wake Yasmine Razaq.
Msimamizi wa kampuni ya Asas Diaries  Fahad Alli akiwa na mshambuliaji Wilfried Bony baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad