Na. Monica Mutoni
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa mwelekeo wa hali ya hewa nchini kwa
kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti mwaka 2018. Taarifa hiyo imetoa
uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa, joto, upepo na mvua,
ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za
hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mamlaka
imeeleza kuwa uwepo kwa hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani
inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi
inatarajiwa katika maeneo ya miinuko ya nyanda za juu Kaskazini
mashariki (Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Nyanda za juu kusini
Magharibi (hususani mkoa wa Njombe) pamoja na maeneo ya miinuko ya mkoa
wa Tanga (hususan wilaya za Lushoto na Bumbuli).
Kuhusu
hali ya mvua na upepo taarifa hiyo imeeleza kuwa maeneo mengi
yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla,pamoja na vipindi vifupi vya upepo
mkali vinatarajiwa kujitokeza katika baadhi ya maeneo. Aidha, vipindi
vya mvua za nje ya msimu vinatarajiwa katika maeneo ya pwani hususan
katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Juni, 2018 na vipindi kadhaa kwa
mwezi Julai, 2018.
Wananchi
wameendelea kushauriwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa ili
kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kama vile hali ya baridi
inayotarajiwa katika maeneo mengi ya nchi hususan maeneo ya miinuko
nakuweza kusababisha kudumaa kwa mazao kama vile ndizi pamoja na mazao
ya nje ya msimu, na kuathiri mifugo. Vile vile, kutokana na hali ya joto
katika bahari ya Hindi kuwa juu ya wastani kiasi, ongezeko la siku
zenye tija katika shughuli za uvuvi katika kipindi cha msimu wa JJA
linatarajiwa.
Kwa taarifa zaidi temebelea tovuti www.meteo.go.tz
No comments:
Post a Comment