HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 28, 2018

MJUMBE WA NEC GACHUMA AWAONGOZA WANANCHI SIMIYU MAZISHI YA DC NA MBUNGE MSTAAFU, KATIBU MWENEZI MKOA WA SIMIYU

Na Stella Kalinga, Simiyu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma amewaongoza wananchi na viongozi wa CCM na Serikali wa mkoa wa Simiyu katika mazishi ya aliyewahi kuwa mbunge wa Bariadi, Mkuu wa Wilaya katika maeneo mbalimbali hapa nchini,ambaye pia alikuwa Katibu wa Itikadi  na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw. Danni Makanga, ambayo yamefanyika katika Mtaa wa  Kidulya Mjini Bariadi .

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Gachuma ametoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huo, huku akiwaasa ndugu na familia kuendelea kuishi maisha ya umoja na kushirikiana.

Aidha, Gachuma amepongeza mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano uliopo kati ya Viongozi wa Chama na Serikali katika masuala yote ikiwa ni pamoja na misiba na akikiri kuwa yeye pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wake(Mara) walioongozana naye wamejifunza jambo hilo kutoka Simiyu.

"Napenda niupongeze uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa namna  mnavyoshirikiana, msiba wa ndugu yetu Makanga mmeubeba wote kwa pamoja  tumeona kuna umoja na ushirikiano kati ya viongozi wa Chama na Serikali hili ni jambo jema sana ,  bahati nzuri nimefuatana na Katibu Mwenezi wangu wa Mkoa utaratibu huu na sisi tunaubeba kama somo" alisema Gachuma.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akitoa salamu za rambirambi ametoa pole kwa familia na kuwaomba ndugu na familia waendelee kuwa wamoja na wasikubali kugawanywa kwa namna yoyote, huku akielezea kuwa CCM imempoteza mtu muhimu makini sana ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika Chama, Serikali na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Yakobo amewashukuru viongozi wa CCM Taifa kwa kutuma mwakilishi, pia akawashukuru wananchi, viongozi wa Chama na Serikali mkoani Simiyu kwa namna walivyoonesha umoja na ushirikiano katika msiba wa Bw. Danni Makanga hali ambayo imeleta heshima kwa Chama na kumfanya marehemu Makanga kuzikwa kwa heshima kama kiongozi wa Chama.

Akimzungumzia marehemu Danni Makanga, Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa amesema tangu marehemu akiwa Mbunge wa Bariadi na Mkuu wa Wilaya katika maeneo mbalimbali na kubainisha kuwa alikuwa kiongozi ambaye kupitia yeye vijana wa sasa wanaweza kujifunza namna ya kuitumikia Serikali na wananchi kupitia yeye.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa pole kwa familia, ndugu na marafiki wa marehemu Danni Makanga huku akisisitiza kuwa viongozi wa Chama na Serikali  Mkoani humo wameonesha ushirikiano tangu walipopata taarifa za msiba mpaka wakati wa mazishi ili kumsindikiza marehemu aliyekuwa kiongozi katika heshima zote za Chama na Serikali.

Akitoa mahubiri wakati wa ibada ya mazishi, Padri wa Kigango cha Mtakatifu Michael Kidulya, Parokia ya Mtakatifu Luka Bariadi, James. Kitasanja amewaasa watu wote kujiandaa kwa kuwa hakuna ajuaye siku ya kufa kwake, huku akiwasisitiza kushika maagizo ya Mungu ikiwa ni pamoja na kuwapenda na kuishi vizuri na watu wote.

Marehemu Danni Makanga alifariki Juni 23 katika ajali iliyohusisha lori na pikipiki kugongana uso kwa uso, ambapo wakati wa uhai wake aliwahi kuwa mbunge, mkuu wa wilaya na mpaka mauti inamkuta alikuwa Katibu wa Itikadi  na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, ameacha mke na watoto watano.
 Vijana wa Green Guard wa CCM akiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga kuelekea eneo la mazishi ambayo yamefanyika katika Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi Mkoani humo.
 Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga likiteremshwa kaburini kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika katika Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi Mkoani humo
 Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, . Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Mara, Christopher Gachuma wakiweka udongo katika kaburi alizikwa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga amabye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi.
 Kutoka kulia  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) kupitia Mkoa wa Simiyu, Gungu Silanga na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Busega, mhe. Tano Mwera na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe wakiteta jambo kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga Mjini Bariadi.
 Padri wa Kigango cha Mtakatifu Michael Kidulya, Parokia ya Mtakatifu Luka Bariadi, James. Kitasanja akitoa mahubiri katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa la aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Danni Makanga ambaye amezikwa Mtaa wa Kidulya Mjini Bariadi mkoani humo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad