HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 21 June 2018

BENKI YA BARCLAYS YAANDA SEMINA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI

Na  Agness Francis, Globu ya Jamii
BENKI ya Barclays Tanzania  imeandaa semina ya siku moja kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wakati na lengo kuu ni kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi wa kufanya biashara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wakati wa benki Ahmed Khamis amesema kuwa semina hiyo ni moja ya mpango wa benki ya Barclays kurudisha baadhi ya faida yake kwa jamii.

"Barclays tunaamini kwenye mpango wa kukua pamoja kwa wateja wafanya biashara wetu.Wateja wetu wameweza kuongeza ujuzi wao jinsi ya kuandaa mpango wa biashara, jinsi ya kutangaza biashara zao, jinsi ya kutunza kumbukumbu na njia bora ya kuomba na kutumia mikopo," amesema Khamis.

Kamesema wamengundua na kutambua njia bora ya kufundisha na kuwaongoza wateja wao hasa wale ambao wanaochukua mikopo na kwamba mafunzo hayo yamekuwa muhimu kwao.
 kwani wameweza kuongeza na kupata ujuzi jinsi ya kutengeneza mpango wa biashara, kukuza biashara zao na kukopa kwa kuongeza kukuza biashara.

Amefafanua semina kama hizo zitaendelea kufanyika nchi nzima na nia ni kuongeza ujuzi kwa wateja wao ikiwa tayari zishafanyika Zanzibar na Arusha.

Khamis amesema taasisi nne za Serikali zimekuwa na fursa ya kutoa mada jinsi wanavyofanya shughuli zao na jinsi ya kuwasaidia wafanya biashara hao.

Akizungumza kwenye semina hiyo Mkuu wa Kitengo cha Kampuni kutoka BRELA Rehema Kitambi amesema usajili wa kampuni umekuwa rahisi kwani kwa sasa inasajili kampuni kupitia kwa njia ya mtandao bila mteja kufika katika ofisi zao.


"Kuna changamoto za kusajili kwa njia ya mtandao kwani kuna baadhi ya watu hawana elimu hiyo huku wengine wakipata changamoto za huduma ya mtandao kulingana na maeneo yao wanavyoishi.

"Ni lazima Mtanzania awe na kitambulisho cha uraia ili kusajili kampuni wakati wengine bado hawajapata vitambulisho.Nawamba wote tuwe pamoja kukubaliana na changamoto hizo  na kwa wale ambao sio raia wanatakiwa kuwa na hati zao za kusafiria,"amesema.
 Afisa Mwandizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Maternus Mallya akitoa mada wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya Barclays Tanzania kwa wajasiriamali wadogo na wa kati 50 kwa lengo ya kuwaongezea ujuzi wa kufanya na kuendesha biashara zao kwa faidi zaidi na pia kuwaongezea ujuzi wa biashara Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha makampuni kutoka BRELA Rehema Kitambi akitoa mada wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya Barclays Tanzania kwa wajasiriamali wadogo na wa kati 50 kwa lengo  la kuwaongezea ujuzi wa kufanya na kuendesha biashara zao kwa faidi zaidi na pia kuwaongezea ujuzi wa biashara Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha makampuni kutoka BRELA, Rehema Kitambi (kushoto) akijadiliana na Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wa kati, Ahmed Khamis wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na benki ya Barclays Tanzania kwa wajasiriamali wadogo na wa kati 50 kwa lengo ya kuwaongezea ujuzi wa kufanya na kuendesha biashara zao kwa faida zaidi na pia kuwaongezea ujuzi wa biashara Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad