HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 11 May 2018

BALOZI WA KUWAIT AZINDUA KISIMA CHA MAJI KATIKA SHULE YA IBNU JAZAR

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem amezindua kisima cha maji safi na salama katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar iliyopo Vikindu Mkoa wa Pwani. Katika hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Picha ya Ndege Mjini Nassoro Ruhulo, Diwani Mstaafu wa Vikindu Al-Hajj Abdalla Bofu pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule hiyo.

Katika hotuba yake fupi mara baada ya ufunguzi wa kisima hicho Mhe. Balozi amesema kuwa kisima hicho ni cha 62 tangu Ubalozi uzindue mradi uliopewa jina la "KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE.

Pia Balozi Al-Najem alikagua madarasa ya Shule, maabara ya Fizia na kituo cha Kompyuta katika Shule ya Ibnu Jazar ambapo aliahidi kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili Shule ikiwa ni hatua ya kuunga mkono sera za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Magufuli katika sekta ya elimu nchini. Shule ya Ibnu Jazar ina idadi ya wanafunzi zaidi ya 800.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akizindua kisima cha  safi na salama katika Shule Ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar iliyopo Vikindu Mkoa wa Pwani.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule Ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar mara baada ya kuzindua kisima cha  safi na salama shuleni hapo
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kisima cha  safi na salama katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar iliyopo Vikindu Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Ibnu Jazar wakimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Al-Najem alipofika shuleni hapo kuzindua  kisima cha  safi na salama shuleni hapo.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al-Najem akikagua maabara ya Fizia na kituo cha Kompyuta kwenye Shule ya Ibnu Jazar iliyopo mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad