HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2017

WAZIRI MWIJAGE :HAKUNA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema hakuna changamoto za biashara nchini bali kinachotokea ni kukosa elimu na taratibu za kufanya biashara.

Mwijage ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Tanzania Growth Trust ambayo awali ilifahamika Gatsby Growth , amesema soko la bidhaa liko la kutosha na hakuna sababu ya kuangalia masoko ya nje wakati ndani  soko bado halijatosholeza mahitaji ya wananchi kupata bidhaa.

Amesema kuwa changamoto  zinazotajwa na wajasiriamali ni zile zinazohusu Shirika la Viwango Tanzania( TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) ambapo kazi ya vyombo hivyo ni kuhakikisha vitu vinavyozalisha vinakuwa na ubora wa kuhimili soko la ndani na nje ya nchi.

Mwijage amesema kukutana katika uzinduzi huo ni pamoja na kueleza namna Serikali inavyoangalia masuala ya viwanda  na wajisiriamali  katika kuzalisha bidhaa ambazo zitahimiri soko la ndani.

 Naye Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Tanzania Grouth Trust(TGT) Oliva Lwena amesema anaishukuru Serikali kwa kutatua changamoto zinazowakabili wajasiriamali nchini.

Pia amesema wao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wajasiriamali wanafanikiwa katika shughuli zao za kimaendeleo na kuongeza ni wakati wa Watanzania kujikita kufanya maendeleo yao.

Ameshauri vijana kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii huku akionesha kutofurahishwa na tabia ya baadhi ya wananchi wanaotumia muda mwingi kucheza mchezo wa kubeti wapate fedha za haraka.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akizungumza katika uzinduzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya  Tanzania Growth (Trust TGT) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Growth Trust (TGT), Oliver Lwena akizungumza juu ya mikakati ya kuwasaidia wajasirimali ili waweze kukua na kuchangia uchumi wananchi jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa  Bodi wa Tanzania Growth Trust (TGT),  Mhandisi Zebadiah Moshi akizungumza juu ya taasisi ya TGT inavyofanya kazi karibu na serikali.
  Sehemu ya wajasiriamali katika uzinduzi wa  TGT.
Bidhaa za wajasiriamali ambao wako katika mwamvuli wa TGT

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad