HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2017

MKUTANO MKUU WA YANGA KUTOA MAAMUZI YA MFUMO WA UENDESHAJI KLABU

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Yanga inatarajia kuwa ya pili kuingia katika mfumo wa hisa kutoka ule wa umiliki wa wanachama kama walivyofanya watani wao wa jadi Simba wiki mbili zilizopita.

Simba iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania na Afrika Mashariki na kati kuingia mfumo huo ambapo Yanga wanatarajiwa kuwa wapili.

Katibu mkuu wa timu ya Yanga, Boniface Mkwasa amesema kikako cha kamati ya Utendaji kilichoketi Disemba 13 kimefikia maamuzi hayo ambapo watasubiri mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika ndani ya miezi mitatu ili kukamilisha jambo hilo.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa alisema wataunda kamati itakayosimamia mchakato wa zabuni ambao kwa mujibu wa katiba yao wanachama wanatakiwa kubaki na asilimia 51 na wawekezaji asilimia 49.

"Kamati ya utendaji imekutana juzi na kupitisha kubadili mfumo wa uendashaji wa klabu kutoka mfumo wa umiliki wa wanachama hadi hisa ambapo mchakato tayari umeanza siku chache zijazo tutatangaza kamati ya kusimama jambo hilo," alisema Mkwasa.

Simba iliingia rasmi kwenye mfumo wa hisa Disemba 3 mwaka huu ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' alifanikiwa kushinda zabuni na atawekeza kiasi cha sh bilioni 20 kwa Wekundu hao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad