Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Utengule, alipowasili kuzindua ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi huku eneo hilo likitolewa na wananchi wa kijiji hicho.Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.(Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizindua
Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha
Utengule.Wanaoshuhudia ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa Wilaya ya
Mbeya, Jesse Shengena (kulia), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza
kuimarisha ulinzi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.
Mhandisi
wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kushoto), akimuelekeza Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati)
ramani ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la
Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Kulia ni Kaimu Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula, akitoa maelezo juu ya
Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi kwa
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (katikati), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi
ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho cha Utengule wilayani
Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Utengule baada ya kuzindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa
ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.Naibu Waziri
aliwashukuru wananchi hao kwa kujitolea eneo la kujengwa ofisi za watumishi na askari wa
jeshi ikiwa ni juhudi zao katika kupambana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao.
No comments:
Post a Comment