Mtanange kati ya Yanga na Mwadui Fc ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku timu zote zikionyesha kusambuliana kwa zamu. kipindi cha pili cha mchezo huo kimeanza hivi punde na Yanga inaongoza kwa bao 2-0 yaliyowekwa kimiani na Mshambuliaji Obrey Chirwa.Globu ya jamii iko uwanjani hapa kukuhabarisha kinachoelezea.
Kikosi cha Mwadui FC.
Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe akipimana ubavu na Malika Ndeule wa Mwadui Fc, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, unaendelea kuchezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga inaongoza kwa bao 1-0.
Kipa wa Mwadui, Shaaban Kado akijiandaa kuupiga mpira.
No comments:
Post a Comment