TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini
Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari
29, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinaeleza kuwa takriban mabehewa 10 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea,aidha imeelezwa kuwa watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.

Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.
“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.
Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyotufikia.
HABARI KWA HISANI YA KIVIS-BLOG
Baadhi ya Mabehewa ya TRENI
ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar
es Salaam, yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29,
2017.
Baadhi ya Mabewa mengine yakionekana kuacha njia
Baadhi ya Abiria waliokuwa wamependa TRENI
ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar
es Salaam,wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29,
2017.
No comments:
Post a Comment