
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akieleza jambo wakati alipotembelea shamba la ng'ombe wa maziwa la MILKCOM TANZANIA LIMITED lililopo Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni leo Januari 4, 2017.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II linakuwa na umeme wa
uhakika ili kuwezesha viwanda na wananchi wa eneo hilo kupata nishati
hiyo.
Alitoa
agizo hilo jana jioni (Jumanne, Januari 3, 2017) wakati alipotembelea
kiwanda cha Milkcom kinachozalisha bidhaa za maziwa na kiwanda cha
Watercom kinachozalisha maji vilivyoko katika kata ya Kisarawe ii
wilayani Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.
“Waziri
wa Nishati ahakikishe eneo hili linapata umeme wa uhakika ili
kuviwezesha viwanda hivi kufanyakazi vizuri jambo litakaloongeza
uzalishaji. Pia wananchi wanaoishi katika maeneo haya nao watanufaika na
upatikanaji wa nishati hiyo,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema amefarijika na jitihada za muwekezaji huyo za kuungamkono
mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya Tanzania kujenga uchumi
wa viwanda utakaoliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025.
Awali,
Msemaji wa Viwanda hivyo, Aboubakar Faraj akisoma taarifa ya viwanda
hivyo kwa Waziri Mkuu alisema moja ya changamoto zinazowakabili ni
pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo linasababisha kupanda
kwa gharama za uzalishaji.
“Punde
umeme unapokatika tunalazimika kutumia majenereta kwa muda mrefu. Hii
husababisha ongezeko la gharama za uzalishaji ambazo huumiza kiwanda kwa
sababu haiwezekani kumtwisha mzigo huu mlaji,” alisema.
Faraji
alisema changamoto nyingine ni miundombinu ya barabara ambayo
usababisha wateja wengi kushindwa kufika kwenye viwanda hivyo kwa
urahisi, hivyo aliiomba Serikali kuwatatulia kero hilo.
Aliongeza
kuwa kwa sasa viwanda hivyo vimeajiri watu zaidi ya 1,800, ambapo
alisema endapo Serikali itawahakikishia upatikanaji wa umeme na barabara
wataongeza ajira kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2018.
Mapema Waziri
Mkuu alizindua wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kisarawe ii
iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom. Wodi hiyo yenye
vyumba vitatu itawapunguzia akinamama kusafiri umbali mrefu kutuata
huduma hiyo.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngombe wa kisasa wakati alipotembelea
shamba la ng'ombe wa maziwa la MILKCOM TANZANIA LIMITED lililopo
Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wilaya ya
Kigamboni leo Januari 4, 2017.

Wananchi wa eneo la Kisarawe Two wilayani Kigamboni wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kukagua wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni ya mafuta ya OILCOM kijijini hapo. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara ya wilaya hiyo Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitazama kitanda wakati alipotembelea wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni ya mafuta ya OILCOM katika ENEO la Kisarawe Two wilayani Kigamboni, Januari 4, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Mhe. Hashim Mgandilwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi wakati alipotembelea maghala ya NFRA, Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017. Kulia kwake ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017. Kulia kwake ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,

No comments:
Post a Comment