Madaktari wa meno wameshutumu utamaduni wa kazini wakisema ugawanyaji wa keki na peremende unachangia matatizo ya kiafya.
Idara ya afya ya meno imesema kuwa watu wanafaa kupunguza ulaji wa keki na biskuti kazini kwa sababu vyakula hivyo vinawafanya kunenepa kupita kiasi mbali na afya mbaya ya mdomo.
Profesa Nigel Hunt amesema kuwa wafanyakazi wanahitaji kubadilisha utamaduni wa kazini. Ili kuweza kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari wafanyakazi wameshauriwa kutumia vyakula hivyo kama chakula cha mchana mbali na kuvificha .
Profesa Hunt, ambaye ni muhadhiri wa chuo kikuu cha Royal College of surgeons ,alisema kuwa huenda wasimamizi wa ofisi hizo wanataka kuwazawadia wafanyakazi, kutaka kusherehekea ama mtu anayeleta zawadi ofisini baada ya likizo hatua inayosababisha vyakula vya sukari nyingi kuingia ofisini.
Lakini amesema kuwa hilo linaathiri afya zaona ni muhimu kufanya uamuzi wa mwaka mpya wa kukabiliana na utamaduni wa vyakula vya sukari.
''Ijapokuwa peremende hizo huenda zikawa na maana ,zinachangia unenepaji wa kupitia kiasi pamoja na afya mbaya ya mdomo,''aliongezea.
Tunahitaji kubadili utamaduni katika afisi zetu ambao unashawishi ulaji wa vyakula vya afya na unawasaidia wafanyikazi kutotumia vyakula vya sukari kama vile, keki, peremende na biskuti. Chanzo: BBC Swahili


No comments:
Post a Comment