Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Shindano la wajasiliamali kwa vyuo vikuu mbalimbali nchini linategemea kuanza hivi karibuni likidhaminiwa na Benki ya Barclays nchini Tanzania.Kupitia benki hiyo kumezundiliwa mpango wake mpya wa udhamini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mratibu wa mradi huo Victor Mnyawami amesema kuwa wataweza kuzunguka vyuo vikuu vyote kwa ajili ya kupata washindani.
“ujasiliamali ni muhimu sana katika uchumi wa taifa hili hivyo ni vyema tukawa na wahitimu wa vyuo vikuu ambao wataweza kujitengenezea ajira zao wenye kuliko kusubiri kuajiriwa” amesema Mnyawami.
Kwa upande wake afisa uhusiano wa Barclays, Hellen Siria amesema kuwa mshindi wa shindano hilo atapata fursa ya kuungana na vijana wengine kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini ujerumani.
Hellen amesema kuwa vijana watakaopata fursa ya kupita kwenye mchujo watapata nafasi ya kupata mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia kujiajiri.
Kiongozi wa Taasisi inayoandaa shindano la wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini, Victor Mnyawami akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na shindano hilo.
Meneja uhusiano wa Benki ya Barclays nchini, Hellen Siria wakijadiliana jambo na Kiongozi wa Taasisi inayoandaa shindano la wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini, Victor Mnyawami kuhusu mchango wa Bank hiyo katika kusaidia jamii hasa wanavyuo.
No comments:
Post a Comment