HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 26, 2017

KOCHA MPYA AZAM AJA NA MBINU MPYA YA KUIVAA SIMBA J'MOSI



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii



Baada ya kutoka na ushindi dhidi ya Cosmo Politan wa magoli  3-1 na kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la FA, Klabu ya Azam , Jumamosi itakuwa kibaruani kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 

Tayari kikosi cha Azam  kimeanza rasmi mazoezi juzi jioni kwa ajili ya kujiandaa na mtanange huo unaotarajiwa kuwa ni wa kisasi kwa pande zote mbili kutokana na aina ya matokeo yaliyotokea katika mechi zao za mwisho walizokutana msimu huu.

Wakati matajiri hao wa Azam Complex wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, Simba nayo itataka kupooza machungu ya kufungwa na Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi (1-0) Januari 13 mwaka huu.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Aristica Cioaba aliingia na mbinu mpya za kuweka fedha mezani ili kuwapa motisha wachezaji wake kufanya mazoezi kwa nguvu ambapo aliwagawa katika makundi manne ya wachezaji sita na kuanza kuwashindanisha.


 Cioaba anatarajiwa kuwa katika benchi la ufundi la Azam katika mchezo huo wa Jumamosi dhidi ya Simba huku akitaka kuweka rekodi ya kutokupoteza mechi hiyo muhimu.


Kuelekea mchezo huo, manahodha wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ na Shomari Kapombe, wametoa neno kwa upande wa wachezaji wenzao namna walivyojithatiti kuibuka na pointi zote tatu dhidi ya wapinzani wao hao.

“Tukikutana na Simba tunakuwa tunacheza mpira wa kujuana na pia wa kuogopana, lakini naamini ni mechi ngumu, watakuwa na mipango yao na sisi tutajipanga kwa upande wetu, naamini tutajituma na tutaweza kupata ushindi,” alisema nyota huyo.

Bocco ataingia kwenye mchezo huo akiwa na rekodi ya aina yake ya kuifunga mabao mengi Simba kuliko mchezaji mwingine yoyote kihistoria, akiwa tayari ameshaziona nyavu zao mara 18 katika mechi za mashindano mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad