Katika picha ni baadhi ya polisi wa kutuliza ghasia wakiwa wamewakamata baadhi ya madereva wa bajaji walio kuwa wakifanya fujo kwenye baadhi ya maeneo mbalimbali hasa eneo la kabwe kwa kuweka mawe barabarani kutokana na mgomo wa kuto endesha shughuli zao mpaka wenzao walio kamatwa na kutuhumiwa na makosa tofauti tofa uti ikiwemo, Leseni ya udereva, Leseni ya bishara pamoja na kupita njia walizo katazwa na mamlaka.
Polisi wakiendelea kuwakamata walio kuwa wakifanya fujo katika eneo la kabwe jijini mbeya majira ya jioni ambapo jeshi la polisi kitengo cha kutuliza ghasia kilisambaratisha madereva wote walio kuwa wakiweka mawe kwenye baadhi ya barabara na kupiga mabomu ya machozi hali iliyo pelekea jiji la mbeya kuwa Kimya kwa muda wa masaa kadhaa.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Baadhi ya wasafiri wakiwa katika gari ya wazi moja kati ya usafiri ulio ibuka kufuatia mgomo huo wa bajaji na matokeo yake kuwanufaisha madereva wa magari binafsi na bodaboda kusafirisha abiria.
#Kamerayamtaakwamtaablog.
No comments:
Post a Comment