Pichani ni kijana anaejishughulisha na kazi ya kuendesha pikipiki inayopakia abiria maarufu kama Bodaboda, akionyesha manjonjo yake na chombo hicho katika Barabara ya Morogoro, eneo la Magomeni Mapipa, Jijini Dar es salaam leo, ikiwa ni kuonyesha ni namna gani ana uzowefu na chombo chake hicho. Jambo hilo lilishangaza wengi waliokuwepo eneo hilo, kwani hakuna alietegemea kuona michezo ya aina hiyo ikifanyika katika barabara kubwa na yenye magari mengi kama hii. Tukio hili na mengine mengi ya namna hiyo, yamekuwa yakifanywa sana na ndugu zetu hawa, na wakati mwingine kupelekea madhara makubwa kwao na wengine kupoteza maisha kutokana na matumizi mabaya ya vyombo hivi na kupelekea nguvu kazi ya taifa kuendelea kupotea. Hiki ni kijipu upele kilichiva kabisa na kinachotakiwa ni kutumbuliwa tu, hivyo wazee wa feva liangalieni jambo hili kwa jicho la tatu, bila hivyo vijana wengi tutawapoteza.
Mbwembwe zikiendela.
No comments:
Post a Comment