HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 6, 2016

SERIKALI YATOA TAMKO KWA WACHIMBAJI WADOGO WA CHUMVI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini prof,Jamse Mdoe (wa pili kushoto) akisomo mikakati mbalimbali ya serikali wakati akifungua akifungua mkutano wa chama cha wazalishaji chumvi wadogo,kushoto ni Mwenyekiti wa  Chama cha Wazalishaji Chumvi  Habibu Nuru na viongozi wengine.

Na Anthony John Globu ya Jamii.

SERIKALI imewataka wachimbaji wadogo wa chumvi kuhakikisha wanazalisha chumvi iliyo na ubora na yenye kiwango cha madini joto ilikuepuka madhara ya kiafya kwa watumiaji. 

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam katika kufungua mkutano wa mwaka wa chama cha wazalashaji chumvi Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof, James Mdoe amesema Serikali inajitahidi kuboresha sheria za sekta ya wachimbaji wadogo na wazalishaji wa chumvi ilikuongeza uzalishaji wa mapato katika Taifa.

Sambamba na hayo Mdoe alifafanua baadhi ya  madhara ya kiafya kwa watumiaji chumvi isiyo na kiwango cha madini joto ni pamoja na kuharibu mimba na kuzaa watoto wenye ulemavu  na madhara mengine ya kiafya.

Katika uzinduzi huo wa wachimbaji wa chumvi,  Prof. Mdoe  alisema katika mwaka huu wa fedha 2016 hadi 2017 wizara yake itakamilisha kutengeneza kituo kimoja cha mfano wa mafunzo ya uzalishaji chumvi.

Tumepanga kituo hicho kijwngwe katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi na kitakuwa ni kiwanda ambacho kina mchakato wote wa namna ya kuzalisha chumvi kwa ubora wa kimataifa.

Hivyo Hivyo Mwenyekiti wa chama hicho cha wachimbaji wadogo wadogo  wa chumvi  Habibu  Nuru ameishukuru serikali kwa kuwasaidia tani 4 za madini joto pamoja na kilo miasaba zilizotolewa kwa wazalishaji hao ilikuweza kuboresha Chumvi.
Wadau mbalimbali walijitokeza kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad